Aug 03, 2016 02:22 UTC
  • Erdogan: Madola ajinabi yalihusika kuratibu mapinduzi

Rais Recep Tayyep Erdogan wa Uturuki ameyataja madola ya nje kuwa yalihusika na kuratibu mapinduzi yaliyofeli nchini humo.

Erdogan amesema Jumanne hii kuwa Magharibi inaunga mkono ugaidi na kwamba senario ya jaribio hilo la mapinduzi nchini kwake iliratibiwa nje ya nchi.  Akizungumza mbele ya hadhara ya wawekezaji wa nchi za nje huko Ankara mji mkuu wa Uturuki, Erdogan ameongeza kuwa tunapaswa kueleza kuwa jaribio hilo la mapinduzi lilifanywa na nchi za nje. Amesema mapinduzi hayo si tukio ambalo lingeweza kuongozwa na kuratibiwa kutoka ndani tu ya nchi.

Rais Recep Tayyib Erdogan wa Uturuki

Rais Recep Tayyib Erdogan amesema kuwa Ankara itasitisha ushirikiano wake wa kistratejiai na Washington iwapo Marekani itaaendelea kumpa hifadhi Fethullah Gulen shakhsia wa kidini anayeipinga serikali ya Uturuki  ambaye yuko uhamishoni nchini Marekani.

Wafuasi wa Rais Erdogan

Uturuki inamtuhumu Fethullah Gulen kuwa alipanga jaribio hilo la mapinduzi la hivi karibuni huko Uturuki. Gulen mwenye umri wa miaka 75 amekanusha kuhusika na jaribio hilo la mapinduzi.

 

 

 

 

 

 

Tags