Wakulima: Mzingiro tulioiwekea Iran unatumaliza sisi wenyewe Wamarekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i141444-wakulima_mzingiro_tulioiwekea_iran_unatumaliza_sisi_wenyewe_wamarekani
Chama cha Wakulima wa Michigan huko Marekani kimeshindwa kujizuia kulalamikia hali ngumu wanayopitia baada ya Marekani kuanzisha vita dhidi ya Iran na kuizingira kiuchumi na kimesema, mzingiro tulioiwekea Iran unatumaliza sisi wenyewe Wamarekani.
(last modified 2026-09-14T07:38:06+00:00 )
Sep 14, 2026 07:37 UTC
  • Wakulima: Mzingiro tulioiwekea Iran unatumaliza sisi wenyewe Wamarekani

Chama cha Wakulima wa Michigan huko Marekani kimeshindwa kujizuia kulalamikia hali ngumu wanayopitia baada ya Marekani kuanzisha vita dhidi ya Iran na kuizingira kiuchumi na kimesema, mzingiro tulioiwekea Iran unatumaliza sisi wenyewe Wamarekani.

Serikali ya Donald Trump inatumia mzingiro wa majini kama njia kuu ya kuongeza mashinikizo ya kiuchumi dhidi ya Iran, lakini takwimu zinaonesha kuwa sera hiyo imeleta matokeo tofauti kabisa na alivyotarajia kwani maisha yanazidi kuwa magumu nchini Marekani na bei ya mafuta inazidi kupanda siku baada ya siku. 

Chama cha Taifa cha Wakulima wa Michigan ambacho ni maarufu kwa jina la mkulima wa kizazi cha sita kutoka familia ya Dence na ambacho kinajishughuliisha na kilimo cha soya na ufugaji kimeshindwa kuvumilia na kimeamua kusema hadharani kwamba: "Vita dhidi ya Iran vimesababisha kupanda gharama za maisha na bidhaa ndani ya Marekani."

Chama hicho kimesema kuwa kinatamani kuwa na rais ambaye ataweza kutatua matatizo ya kiuchumi na kuwaunga mkono wakulima pamoja na familia zao hasa wakati huu ambapo wanakabiliana na changamoto kubwa za kiuchumi, usafirishaji wa mazao na kupoteza mikataba minono.

Mkulima mwingine kutoka California amelitaja suala la kupanda bei ya dizeli hadi dola 6 kwa galoni huko Marekani kwamba limevuruga maisha yao na kuongeza gharama za usafirishaji wa mazao ya kilimo sambamba na sera mbovu za ushuru za Trump, ambazo zimeongeza kwa kiasi kikubwa gharama za pembejeo za kilimo. Alibainisha kuwa hali ya kutokuwa na uhakika katika biashara ya kimataifa iliyosababishwa na ushuru huo imewalazimu wakulima wa Marekani kupoteza mikataba mingi ya mauzo. Kwa mujibu wa takwimu rasmi, bei ya mafuta nchini Marekani imepanda kwa asilimia 60 ikilinganishwa na kabla ya dola hilo la kibeberu kuanzisha vita vya kivamizi dhidi ya Iran.

Huku hayo yakiripotiwa, shirika la GasBuddy la Marekani ambalo linafuatilia bei za mafuta nchini humo limesema kuwa, hivi sasa kila galoni moja la mafuta ya dizeli linauzwa kwa dola 9.999 katika jimbo la California. 

Hadi wakati linatoa ripoti hiyo, shirika hilo lilikuwa linaendelea kufuatilia mfumuko wa bei ya mafuta katika majimbo mengine ya Marekani.