Mamillioni ya Wamarekani wanyimwa haki ya kupiga kura
https://parstoday.ir/sw/news/world-i19117-mamillioni_ya_wamarekani_wanyimwa_haki_ya_kupiga_kura
Huku matokeo yasiyo rasmi ya uchaguzi wa rais Marekani yakionyesha kuwa Donald Trump wa chama cha Republican amepata ushindi dhidi ya mshindani wake wa chama cha Democrat Hillary Clinton, imebainika kuwa idadi kubwa ya Wamarekani wamenyimwa haki yao ya kupiga kura.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 09, 2016 08:14 UTC
  • Mamillioni ya Wamarekani wanyimwa haki ya kupiga kura

Huku matokeo yasiyo rasmi ya uchaguzi wa rais Marekani yakionyesha kuwa Donald Trump wa chama cha Republican amepata ushindi dhidi ya mshindani wake wa chama cha Democrat Hillary Clinton, imebainika kuwa idadi kubwa ya Wamarekani wamenyimwa haki yao ya kupiga kura.

Kwa wastani, kati ya kila Wamarekani 40 mtu moja anahudumia kifungo cha zaidi ya mwaka mmoja gerezani na hivyo kunyimwa haki ya kupiga kura.

Aidha katika zaidi ya majimbo 12 ya Marekani watu waliowahi kuhudumu kifungo jela na sasa wameachiliwa huru hawana haki ya kupiga kura. Katika  jimbo la Florida, Wamarekani milioni 1.5 pamoja na kuwa wanawajibishwa kulipa kodi lakini hawana haki ya kupiga kura. Aghalabu ya walionyimwa haki ya kupigwa kura ni Wamarekani wenye asili ya Afrika.

Kwa kuzingatia idadi kubwa ya raia wa Marekani walionyimwa haki ya kupiga kura, ukweli mchungu na uliowazi ni kuwa, Marekani kama nchi kubwa zaidi ya kibepari duniani imegawanyika kaitka makundi mawili ya walio nacho na wasio nacho yaani Haves and the Have Nots. Ukweli huu mchungu hauko tu katika sekta ya kiuchumi na kijamii bali pia katika uga wa kisiasa.

Kundi la wasio nacho Marekani linajumuisha Wamarekani wenye asili ya Afrika, Wamarekani wenye asili ya Amerika ya Latini, masikini na wasio na nyumba,

Katika majimbo manne ya Marekani, kati ya kila Wamarekani weusi watano, mmoja ana historia ya kufungwa jela na hivyo hapati haki ya kupiga kura.

Kinyume na madai ya  Marekani kuhusu uhuru na haki za binadamu, tunaona namna Wamarekani Wenye asili ya Afrika, pamoja na kuwa idadi yao ni mamilioni, hawana nafasi muhimu katika mfumo wa nchi hiyo na wanabaguliwa kwa siri na wazi wazi.

Rangi ya ngozi ina nafasi muhimu katika kuainisha ni nani ataweza kufanikiwa kimaisha Marekani na ni nani atabaki nyuma. Wamarekani wenye asili ya Afrika ni asilimia 13 ya watu wote wa Marekani lakini hawana utajiri, elimu na maisha bora katika jamii. Aidha wanakabiliwa na masaibu pamoja na matatizo mengi katika jamii.

Hivi sasa imebainika kuwa hata katika  masuala ya kimsingi kabisa ya haki za mtu binafsi yaani haki ya kupiga kura, Wamarekani wenye asili ya Afrika wanabaguliwa.

Ukandamizaji wa Wamarekani weusi

Umasikini, ukosefu wa nyumba na makazi ni jambo ambalo pia limepelekea idadi kubwa ya Wamarekani wanyimwe haki ya kupiga kura. Aidha idadi kubwa ya Wamarekani wasio na kitambulisho pia wamenyimwa haki ya kupiga kura.

Takwimu zinaonyesha kuwa mtu mmoja katika kila Wamarekani 10 hana kitambulisho na hivyo hawezi kupiga kura. Aidha Wamarekani milioni nne wanaoishi katika ardhi zinazotawaliwa na Marekani kama vile Puerto Rico, Guam, Kisiwa cha Marina Kaskazini, Visiwa vya Virgin na Samoa hawana haki ya kupiga kura.

Kwa hivyo, katika nchi ambayo inadai kuongoza kaitka uhuru na haki za binadamu idadi kubwa ya raia wake hawana haki ya kipiga kura na kuainisha kiongozi wanayemtaka. Hata miongoni mwa watu waliotimiza masharti ya kupiga kura Marekani, yaani milioni 218 ni watu milioni 146 tu ndio waliojisajili kupiga kura.