Myanmar yazuia misaada ya Malaysia kuwafikia Waislamu Warohingya
https://parstoday.ir/sw/news/world-i22441-myanmar_yazuia_misaada_ya_malaysia_kuwafikia_waislamu_warohingya
Utawala wa Myanmar unaendelea kuzuia msafara wa meli za Malaysia zinazosheheni misaada ya dharura kwa ajili ya Waislamu wa kabila la Rohingya huku uhusiano wa nchi mbili hizo ukiendelea kuzorota.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 30, 2016 12:23 UTC
  • Myanmar yazuia misaada ya Malaysia kuwafikia Waislamu Warohingya

Utawala wa Myanmar unaendelea kuzuia msafara wa meli za Malaysia zinazosheheni misaada ya dharura kwa ajili ya Waislamu wa kabila la Rohingya huku uhusiano wa nchi mbili hizo ukiendelea kuzorota.

Msafara huo ulikuwa uondoke Malaysia kuelekea katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar ambapo Waislamu wa kabila la Rohingya wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha. Msafara huo ulipangiwa kuondoka Malaysia Januari 10 ukiwa na shehena ya tani 1,000 za mchele, dawa na mahitajio mengine ya dharura kwa ajili ya Waislamu  wa Rohingya lakini wakuu wa Myanmar wamekataa kutoa idhini kwa meli hiyo.

Malaysia imekuwa ikiikosoa vikali serikali ya Myanmar kwa kuwakandamiza Waislamu katika jimbo la Rakhine ambapo katika miezi ya hivi karibuni maelfu ya Waislamu wanaripotiwa kuuawa kiholela huku wengine laki tatu wakilazimika kukimbia makazi na nyumba zao.

Maandamano ya Waislamu wa Bangladesh kuunga mkono Waislamu wa Myanmar

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Waislamu wa kabila la Rohingya ni jamii ya wachache duniani inayodhulumiwa na kunyongeshwa zaidi. Serikali ya Myanmar inakataa kuwapa haki za uraia Waislamu hao ambao idadi yao ni zaidi ya watu milioni moja na laki tatu.

Katika miaka ya karibuni, Waislamu wengi wa kabila la Rohingya nchini Myamnar wameuawa au kulazimika kuhama makazi yao na kuwa wakimbizi katika nchi za Thailand, Malaysia na Indonesia kutokana na mashambulio ya maafisa wa usalama na Mabudha wenye misimamo ya kufurutu mpaka wanaoungwa mkono na serikali ya nchi hiyo