Jan 13, 2017 08:10 UTC
  • HRW: Donald Trump ni tishio kwa haki za binadamu

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema kuchaguliwa Donald Trump kuwa Rais wa Marekani ni tishio lisilo na mfano kwa haki za binadamu.

Katika ripoti yake ya kila mwaka iliyotolewa jana, Huma Rights Watch imemtaja Trump kama mtu asiyeheshimu demokrasia na misingi ya sheria.

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limesema kampeni za Trump ziligubikwa na matamshi ya chuki na kibaguzi na alidhihirisha kipindi hicho kuwa yeye sio mwanasiasa mwenye uwezo wa kuwavumilia watu wengine.

Wamarekani wakiandamana kupinga ushindi wa Trump

Jamii za walio wachache nchini Marekani zilifanya maandamano kupinga ushindi wa Trump, huku hujuma zinazotokana na chuki na ubaguzi zikiripotiwa kuongezeka nchini humo tangu atangazwe mshindi wa uchaguzi huo.

Itakumbukwa kuwa, Rais-mteule wa Marekani Donald Trump amewateua watu wenye chuki na Uislamu kuhudumu katika Ikulu ya White House, jambo linaloashiria mwendelezo wa sera zake za chuki ambazo zimewatia hofu Waislamu nchini humo.

Trump anatazamiwa kuapishwa kama rais wa 45 wa Marekani Januari 20, chini ya wingu la hofu kwa watu wa jamii za wachache nchini humo.

Tags