Athari mbaya za utumiaji wa silaha mpya za Marekani huko Afghanistan
Hatua ya Marekani na kutumia bomu kubwa zaidi lisilo la nyuklia huko Aghanistan imekabliwa na radiamali kali ya duru mblimbali nchini Afghanistn na katika eno hili kwa ujumla.
Rais wa zamani wa Afghanistan, Hamid Karzai amelaani hatua hiyo na kuwataka Waafghani na viongozi wa nchi hiyo kuzuia jinai kama hizo za Marekani. Karzai amesisitiza kuwa, utumiaji wa bomu kubwa zaidi lisilo la nyuklia duniani katika mkoa wa Nangarhar si vita dhidi ya ugaidi bali ni majaribio ya silaha mpya na hatari sana za Marekani katika ardhi ya Afghanistan.
Jeshi la Marekani lilmefanyia majaribio bomu kubwa zaidi lisilo la nyuklia la nchi hiyo kwa kushambulia viunga vya mji wa Achin katika mkoa wa Nangarhar nchini Afghanistan na kuua watu 36. Bomu hilo linaloitwa “Mama wa Mabomu Yote”, lina uzito wa tani 11 za mada za milipuko ya TNT.
Japokuwa inasemwa kuwa bomu hilo limetumiwa kwa lengo la kupambana na kundi la kigaidi la Daesh lakini wachambuzi wengi wa masuala ya kisiasa na kiusalama wanaamini kuwa, kukabiliana na ugaidi nchini Afghanistan hakuhitaji utumiaji wa bomu kubwa kuliko yote duniani. Wakati wa uvamizi na mashambulizi ya Marekani dhidi ya Afghanistan hapo mwaka 2001 katika kipindi cha utawala wa Warepublican, jeshi la Marekani lilifanyia majarabio maelfu ya mabomu ya aina mbalimbali huko Afghanistan hususan katika milima ya Torabora. Hivi sasa pia Warepublican wameshika tena madaraka huko Marekani na wameanza kufanyia majaribio kizazi kipya cha mabomu yasiyo ya nyuklia huko Afghanistan.
Kwa kutilia maanani kwamba, kwa sasa Marekani na Russia zimeanza duru mpya ya mashindano huko Afghanistan, inaonekana kuwa, baada ya kuishambulia Syria, serikali ya Washington imerusha bomu lenye nguvu kubwa zaidi huko Afghanistan kwa shabaha ya kuonesha misuli na nguvu zake mbele ya Moscow. Hii ni pamoja na kwamba, kuangamiza ugaidi huko Afghanistan au eneo lolote jingine, hakuhitaji utumiaji wa bomu kubwa kuliko yote duniani, bali kinyume chake, mauaji ya raia wasio na hatia na kuzidisha chuki dhidi ya Marekani katika maeneo mbalimbali ya dunia kunaimarisha zaidi nafasi ya makundi ya kigaidi. Hii ni kwa sababu, makundi hayo yatachukua hatua ya kusajili na kuwashawishi vijana kujiunga nayo kwa kutumia nara ya kulipiza kisasi na kuwafukuza wavamizi wa kigeni katika nchi yao.
Marekani imeishambulia Afghanistan kwa kutumia bomu lake kubwa zaidi wakati katika kipindi chote cha miaka 16 ya kuikalia kwa mabavu nchi hiyo haijachukua hatua yoyote ya kuijenga upya nchi hiyo iliyoharibwa na vita au hata kuimaisha kikosi chake cha jeshi la nga. Mbali na hayo, utumiaji wa mabomu kama hayo huko Afghanistan ni kielelezo kwamba, Marekani imeifanya nchi hiyo kama eneo la kufanyia majaribio ya silaha zake mpya.
Kujitokeza kwa kundi la kigaidi la Daesh huko Afghanistan kumeipa Marekani fursa na kisingizio cha kuzidisha idadi ya askai wake nchini humo na kutunisha misuli kwa nchi hasimu na wapinzani katika eneo la mashariki mwa Asia. Katika mazingira hayo rais wa zamani wa Afghanistan, Hamid Karzai sambamba na kukosoa vikali mwenendo wa kuziishwa idadi ya askari wa Marekani nchini humo, amesema kuwa kujitokeza kundi la kigaidi la Dash katika ardhi ya Afghanistan licha ya kuwepo jeshi la Marekani nchini humo kwa miaka mingi, ni jambo linalotia shaka. Karzai anasisitiza kuwa, kundi hilo linatumiwa kama wenzo wa kuhalalisha suala la kuendelea kuwepo askari wa Marekani katika nchi hiyo na kuitumia Afghanistan kama maabara ya majaribio ya silaha na mabomu ya Marekani.