May 14, 2017 16:23 UTC
  • Wamarekani wazidi kupigana risasi, 55 wauawa na kujeruhiwa masaa 24 yaliyopita

Mauaji ya kiholela na ukatili wa kupigana risasi unaendelea kuitesa jamii ya Marekani kiasi kwamba matukio 61 yaliyotokea masaa 24 yaliyopita yamepelekea watu wasiopungua 15 kuuawa na wengine 40 kujeruhiwa kwa risasi katika majimbo tofauti ya Marekani.

Shirika la habari la IRIB limenukuu ripoti ya kituo cha kusajili takwimu za machafuko ya kutumia silaha nchini Marekani ikisema kuwa, polisi wa Boston makao makuu ya jimbo la Massachusetts wameripoti habari ya kujeruhiwa watu wawili barabarani mjini humo.

Katika tukio jingine lililotokea kwenye jimbo la Michigan, watu waliokuwa kwenye sherehe waliwalazimisha baadhi ya wageni waondoke eneo hilo, hata hivyo walikataa hapo hapo yakatokea mapigano ya kutumia silaha. Wageni wawili wamejeruhiwa kwenye tukio hilo. Huko Virginia pia, polisi wa Marekani wanafanya uchunguzi kuhusu shambulio la risasi lililofanyika kwenye hoteli moja na kujeruhi watu watatu.

Mwanamme mmoja ameuawa na mwanamke mmoja kujeruhiwa katika ufyatulianaji risasi uliotokea katika nyumba moja huko Dunnville, Kentucky, Marekani. Polisi wamewaomba majirani wa nyumba hiyo wawasaidie kuwakamata wahalifu.

Katika jimbo la Pennsylvania la Marekani pia, baba mmoja mwenye umri wa miaka 60 amempiga risasi na kumuua binti wa miaka 18 na baadaye kujipiga risasi mwenye na kujiua kwa sababu ambazo hadi sasa hazijajulikana.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi zinazotolewa na serikali ya Marekani, kiwango cha uhalifu nchini humo kinazidi kwa asilimia 20 ya uhalifu unaofanyika katika nchi nyingine zilizoendelea. Tab'an kiwango cha uhalifu huko Marekani ni kikubwa mno ikilinganishwa na takwimu rasmi zinazotolewa na serikali.

Tags