Mikono ya Trump imetapakaa damu za Waislamu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i29444-mikono_ya_trump_imetapakaa_damu_za_waislamu
Qari Abdul Rahman Navarzi, mmoja wa maulama wakubwa wa Kisuni nchini Pakistan, amekosoa vikali kitendo kiovu cha utawala wa Aal-Saud cha kumwalika Rais Donald Trump wa Marekani ambaye mikono yake imetapakaa damu za Waislamu kwenda ardhi ilipo nyumba ya Mwenyezi Mungu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 22, 2017 22:49 UTC
  • Mikono ya Trump imetapakaa damu za Waislamu

Qari Abdul Rahman Navarzi, mmoja wa maulama wakubwa wa Kisuni nchini Pakistan, amekosoa vikali kitendo kiovu cha utawala wa Aal-Saud cha kumwalika Rais Donald Trump wa Marekani ambaye mikono yake imetapakaa damu za Waislamu kwenda ardhi ilipo nyumba ya Mwenyezi Mungu.

Abdul Rahman Navarzi ameyasema hayo katika mazungumzo na Redio Tehran na kusema kuwa, uamuzi huo wa kumwalika rais wa Marekani ni kitendo cha jinai ambacho kimefanywa na utawala haramu wa Saudia.

Seikh Abdul Rahman Navarzi, mmoja wa maulama wakubwa wa Kisuni nchini Pakistan

Ameongeza kwa kusema kuwa, katika historia ya Uislamu hakukuwahi kushuhudiwa kitendo kama cha Saudia kwa kumwita kiongozi wa kikafiri kwenda ilipo nyumba ya Mwenyezi Mungu kwa kile kinachosemwa kuwa ni kutatua matatizo ya Waislamu na kisha kumtaka kiongozi huyo kutoa msaada wa kuwaangamiza Waislamu wanaotamka shahada mbili. Qari Abdul Rahman Navarzi, ambaye ni imamu wa msikiti wa jamaa katika jimbo la Baluchistan nchini Pakistan ameweka wazi kwamba, kikao cha Riyadh ambacho hakikuwa na maslahi yoyote kwa Uislamu, ni njama za maadui wa dini hii na kwa hakika kikao hicho kimezitonesha vikali nyoyo za Waislamu duniani.

Mtawala wa Saudia mshirika mkubwa wa Marekani na Israel

Amesisitiza kuwa, Marekani siku zote ni adui wa Qur'an na umma wa Kiislamu na kwamba watawala wa Saudia ni vibaraka wa Marekani na Uingereza. Amemalizia kwa kusema kuwa, ikiwa Washington itaendeleza uungaji mkono wake kwa Saudia, basi bila shaka wananchi watausambaratisha utawala wa kidikteta wa Aal Saud.