PEW: Waislamu wataendelea kuongezeka kwa kasi duniani
Shirika moja la utafiti nchini Marekani limesema uchunguzi umebaini kuwa, idadi ya Waislamu itazidi kuongezeka kwa kasi duniani.
Katika utafiti wake wa hivi karibuni, PEW imechapisha matokeo ya uchunguzi kuhusu idadi ya wafuasi wa dini kubwa duniani. Uchunguzi ambao umebaini kuwa, dini tukufu ya Uislamu, pamoja na changamoto za sasa, inastawi kwa kasi kuliko dini zingine zote duniani.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa PEW, hadi kufika mwaka 2010, idadi ya Waislamu duniani walikuwa bilioni moja, milioni 599 na laki saba yaani asilimia 23 ya wafuasi wa dini zote duniani.
Kwa mujibu wa utabiri wa PEW, ifikapo mwaka 2050, idadi ya Waislamu itakuwa imefika bilioni mbili, milioni 761 na laki 480 yani asilimia 29 ya wafuasi wa dini zote duniani.

Kwa mujibu wa utafiti huo, ifikapo mwaka 2050, idadi ya Waislamu na Waksirsto duniani itakuwa takriban sawa.
Katika uchunguzi wake huo, taasisi ya Kimarekani ya PEW imesema ifikapo mwaka 2050, Uislamu utakuwa dini ya pili kwa ukubwa Marekani baada ya Ukristo. Aidha kwa mujibu wa PEW, barani Ulaya Waislamu watakuwa asilimia 10 ya wakaazi wote wa bara hilo.