Jun 06, 2017 03:27 UTC
  • Marekani yatishia kujiondoa kwenye Baraza la Haki za Binadamu la UN

Marekani inatazamiwa kutoa ishara leo Jumanne juu ya uwezekano wa kujiondoa kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuukingia kifua utawala haramu wa Israel.

Nikki Haley, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amesema utawala wa Rais Donald Trump utaamua mwishoni mwa mwezi huu baada ya mkutano wa  Baraza la Haki za Binadamu la UN mjini Geneva iwapo Marekani itajiondoa au la kwenye baraza hilo ikishinikiza kufanyike marekebisho.

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa Marekani amesema miongoni mwa marekebisho ambayo Washington inataka yafanyike katika baraza hilo ni kufutwa kwa sera eti zilizo dhidi ya Israel.

Marekani imelitaka baraza hilo kuacha tabia ya kuukosoa kila mara utawala wa Kizayuni wa Israel. Baraza hilo la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limepasisha maazimio zaidi ya 70 ya kulaani ukiukaji wa haki za binadamu wa Israel.

Trump, Netanyahu na Mfalme Salma wa Saudia

Marekani imekuwa ikidai kuwa ni miongoni mwa nchi zenye mfumo wa demokrasia na hata kwenda mbali zaidi kudai kuwa eti ni mtetezi wa haki za binadamu. Hii ni katika hali ambayo, wadadisi wa mambo wanasema Marekani imekuwa na utendaji mbovu na wa kundumakuwili uliojaa sera za kibaguzi kuhusu masuala ya haki za binadamu.

Washington imekuwa kimya kuhusu jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina ambao ardhi zao zinakaliwa kwa mabavu; sambamba na kufumbia macho ukiukaji wa haki za binadamu nchini Saudi Arabia na hata mauaji ya raia wa Yemen yanayofanywa na utawala wa Aal-Saud.

Tags