Jun 18, 2017 07:46 UTC
  • Wamarekani wazidi kupigana risasi na kuuana ovyo

Kanali ya habari ya Press TV imeripoti kuwa, kwa wastani, kila mwezi hutokea mashambulizi 27 makubwa ya silaha nchini Marekani.

Katika ripoti yake ya jana Jumamosi, televisheni hiyo imesema kuwa, ufyatulianaji risasi mkubwa husababisha maafa mengi nchini Marekani ikiwa ni pamoja na kuchochea mashambulizi ya kiholela kwenye maeneo ya umma na kusababisha maafa ya roho na mali.

Maelfu ya watu huuawa na kujeruhiwa kwa risasi risasi katika maeneo tofauti ya Marekani kila mwaka.

Takwimu zinaonesha kuwa, raia wa Marekani ndiyo jamii inayomiliki silaha nyingi zaidi nyepesi kuliko jamii zote duniani kiasi kwamba kuna silaha 90 kwa kila watu 100 nchini humo.

Kupigana risasi na mauaji ya kiholela ni jambo la kawaida nchini Marekani

 

Licha ya asasi za kiraia kufanya jitihada kubwa za kupigania kupigwa marufuku umilikaji silaha ovyo nchini Marekani, lakini lobi za mashirika ya kutengeneza silaha zinazuia kuwasilishwa muswada bungeni wa kupunguza kiwango cha kumiliki silaha nchini humo.

Mauaji ya kiholela ni jambo la kila siku nchini Marekani. Mapema mwezi huu wa Juni watu 12 waliuawa na kujeruhiwa kwa risasi katika wilaya ya Orlando, ya jimbo la Florida nchini Marekani.

Duru za kiusalama nchini humo ziliripoti kuwa, tukio hilo lilifanyika siku Jumatatu ya tarehe 5 Juni katika sehemu ya kazi, ambapo watu watano waliuawa na wengine saba kujeruhiwa.

Polisi walisema kuwa tukio hilo lilichochewa na ugomvi miongoni mwa wafanyakazi katika eneo hilo la viwandani karibu na barabara za Forsyth na Hanging Moss.

Tags