Jul 13, 2017 15:09 UTC
  • Wamarekani wazidi kufyatuliana risasi ovyo, 27 wauliwa katika maeneo tofauti

Kituo cha kusajili takwimu zinazotokana na vitendo vya utumiaji silaha nchini Marekani kimeripoti kuwa, watu 27 wameuawa kwa risasi katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Kituo hicho kimeripoti leo kuwa, vitendo vya ufyatuaji risasi vimeripotiwa mara 63 katika muda wa masaa 24 yaliyopita kwenye maeneo tofauti nchini Marekani na kusababisha vifo vya watu 27 na kujeruhi wengine 36. 

Vitendo vya kupigana risasi kiholela vimeripotiwa zaidi katika majimbo ya Pennsylvania, Florida, New York na Indiana. 

Kituo cha kusajili takwimu zinazotokana na vitendo vya utumiaji silaha za moto nchini Marekani aidha kimeripoti kuwa, risasi zimefyatuliwa mara 178 katika muda wa masaa 48 yaliyopita katika miji na majimbo mbalimbali nchini humo; ambapo watu 57 wameuawa na wengine 92 kujeruhiwa katika matukio hayo.

Karibu kila raia Marekani anamiliki silaha ya moto

Maeflu ya watu kila mwaka wanauawa na kujeruhiwa kutokana na kupigwa risasi kiholela katika maeneo mbalimbali nchini Marekani. Ripoti rasmi zinaonyesha kuwa kuna karibu silaha za moto milioni 270 hadi 300 nchini Marekani; ambapo takribani kila mtu anamiliki silaha moja. 

Wafuatilia wa matukio hayo ya kuuana ovyo nchini Marekani wanasema kuwa kesi nyingi huwa haziripoti na vyombo kama hivyo rasmi vya serikali ya Marekani vinachuja sana habari za mauaji ya kila siku ya kiholela yanayotokea nchini humo.

Tags