Sep 16, 2017 07:07 UTC
  • Russia: Marekani na Ulaya zisicheze na moto

Mkuu wa Baraza la Federesheni ya Russia amewatahadharisha mafisa wa serikali za Washington na nchi za Ulaya kukabiliana na nchi hiyo na kusema, siasa zilizodhidi ya Russia za Marekani ni sawa na kucheza na moto.

Valentina Matvienko amesema kuwa, Washington inapaswa kutambua kwamba, kukabiliana na Russia ni kucheza na moto kwa sababu ni kukabiliana na nchi yenye hazina kubwa zaidi ya makombora na silaha za nyuklia na yenye jeshi lenye nguvu kubwa zaidi duniani. 

Matvienko ameongeza kuwa, Moscow daima imekuwa ikikabiliana na siasa za kiungiliaji kati na kibeberu za Marekani na nchi za Magharibi na kwa sababu hiyo uhasama wao dhidi ya Russia unaoongezeka. 

Mfumo wa makombora wa S-400 wa Rassia

Mkuu wa Baraza la Federesheni ya Russia ameashiria migogoro ya Libya, Syria na Mashariki ya Kati na kusema kuwa, sababu kuu ya migogoro yote hiyo ni uingiliaji kati wa nchi za Magharibi katika masuala ya ndani ya nchi hizo na kwamba uingiliaji huo wakati mwingine unapelekea kutokea mpambano wa kisiasa na kiuchumi na hata kuhamasisha mapinduzi na mapigano ya kijeshi. 

Mivutano katika husiano wa Marekani na Russia ambayo ilianza  baada ya kutokea mapigano huko mashariki mwa Ukraine, imeshadidi zaidi katika miezi ya hivi karibuni hususan baada ya uchaguzi wa Rais wa Marekani na madai kwamba Russia iliingilia zoezi hilo.  

Tags