Jan 17, 2018 08:11 UTC
  • Korea Kusini: Tafadhali Marekani msituharibie mazungumzo na Korea Kaskazini

Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini ameitaka Marekani kutochafua nga ya mazungumzo yake na Korea Kaskazini na hivyo kuzuia kufanyika kwa namna bora michuano ya Olimpiki ya msimu wa baridi nchini humo.

Kang Kyung-wha ameyasema hayo alipokutana na wawakilishi wa Kongresi ya Marekani mjini Seoul na kusema kuwa, katika mazingira ya sasa hatua nzuri ni Washington kuzingatia maslahi ya Korea Kusini kwa kuunga mkono michuano hiyo ifanyike katika anga ya amani na mafanikio bila kuingilia mazungumzo yanayoendelea. Kadhalika ameionya Marekani kwa kuikumbusha indhari ya viongozi wa Korea Kaskazini waliotahadharisha kwamba, iwapo Rais Donald Trump ataingilia mazungumzo hayo na kuifanya Korea Kusini kama mwakilishi wake katika mazungumzo hayo, basi Pyongyang itajiengua kutoka katika michuano hiyo. 

Mazungumzo ya kidiplomasia kati ya Korea mbili

Kang Kyung-wha ameongeza kwamba, hadi sasa mazungumzo kati ya nchi yake na Korea Kaskazini yanaendelea katika anga chanya kuhusiana na utumaji wa timu za michezo katika msimu huu wa baridi. Duru ya 23 ya michuano ya Olimpiki ya msimu wa baridi itaanza tarehe 9 hadi 25 mwezi ujao wa Februari, huku michuano ya watu wenye ulemavu ikianza tarehe 9 hadi 18 mwezi Machi mwaka huu katika mji wa Pyeongchang, Korea Kusini.

Tags