Jul 30, 2018 04:40 UTC
  • Wamarekani waendelea kuuana, watu 71 wauawa kwa kupigwa risasi

Kituo cha kuorodhesha takwimu za matukio ya ukatili wa utumiaji silaha za moto nchini Marekani, kimetangaza kwamba jumla ya watu 71 wameuawa kwa kupigwa risasi katika maeneo tofauti ya nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na kituo hicho Jumapili ya jana imesema kuwa, jumla ya matukio 75 yalijiri katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita katika majimbo tofauti ambapo kutokana na hujuma hizo watu 33 wameuawa na wengine 53 wamejeruhiwa. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mengi ya matukio hayo ya ufyatulianaji risasi yametokea katika majimbo ya Wisconsin, Pennsylvania, Tennessee na Illinois. Kadhalika kituo cha kuorodhesha takwimu za matukio ya ukatili wa utumiaji silaha za moto nchini Marekani, kimeripoti kwamba, katika kipindi cha masaa 48 yaliyopita kumejiri matukio 191 ya ufyatulianaji risasi katika majimbo tofauti ya Marekani ambapo watu 71 wameuawa na wengine 122 wamejeruhiwa.

Trump amekataa kupitisha sheria ya kudhibiti matumizi ya silaha za moto nchini Marekani

Inafaa kuashiria kuwa, kwa mwaka maelfu ya watu huuawa nchini Marekani kutokana na matukio ya ufyatuaji risasi katika maeneo tofauti ya nchi hiyo inayojinadi kuwa polisi ya dunia. Hayo yanajiri katika hali ambayo hadi sasa serikali ya nchi hiyo imekataa kupitisha sheria ya kudhibiti silaha za moto, licha ya kutolewa mito mbalimbali inayoitaka serikali hiyo kuchukua hatua hiyo.

Tags