Aug 06, 2018 13:05 UTC
  • Seneta Bernie Sanders: Trump ana maradhi ya kusema uongo

Seneta wa jimbo la Vermont nchini Marekani, Bernie Sanders amemkosoa vikali Rais Donald Trump wa nchi hiyo kwamba, anawahadaa wapiga kura kwa kuwaambia uongo.

Sanders ambaye ni seneta wa kujitegemea anayeshirikiana na chama cha Democrat amesema kwamba Trump ana maradhi ya kusema uongo  na anawahadaa wapiga kura wa tabaka wa wafanyakazi kwa maneno ya uongo.

Bernie Sanders, Seneta wa jimbo la Vermont nchini Marekani.

Seneta Bernie Sanders ameyasema hayo katika mkutano wa uchaguzi jimbo la Michigan ambapo sambamba na kuashiria harakati zilizofanywa na rais huyo kwa ajili ya kufuta mpango wa afya wa Obama Care na kadhalika kupitisha sheria mpya ya ushuru ambayo inawanufaisha watu matajiri amesema: "Wakati Trump alipofika jimbo la Michigan aliwahutubia wakazi wa mji huo na wa majimbo mengine ya Marekani kwamba, atafanya juhudi za kuboresha huduma za afya na matibabu, lakini kumbe yalikuwa maneno ya uongo tu." Mwisho wa kunukuu.

Gazeti la Washington Post la tarehe pili Agosti liliandika kuwa,  katika kipindi cha siku 558 zilizopita za urais wake, Trump amekwishasema uongo au madai yasiyo na ukweli mara 4,229.

Tags