Cohen: Trump alisema watu weusi ni wapumbavu, hawawezi kumpigia kura
https://parstoday.ir/sw/news/world-i49254-cohen_trump_alisema_watu_weusi_ni_wapumbavu_hawawezi_kumpigia_kura
Wakili wa zamani wa Rais Donald Trump wa Marekani amesema rais huyo aliwahi kusema kuwa, watu weusi au wenye asili ya Afrika ni wapumbavu sana.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 03, 2018 23:06 UTC
  • Cohen: Trump alisema watu weusi ni wapumbavu, hawawezi kumpigia kura

Wakili wa zamani wa Rais Donald Trump wa Marekani amesema rais huyo aliwahi kusema kuwa, watu weusi au wenye asili ya Afrika ni wapumbavu sana.

Michale Cohen mpambe na wakili wa zamani wa Trump ameliambia jarida la Vanity Fair kuwa Trump alimfahamisha wazi kuwa, "watu weusi ni wapumbavu sana kiasi kwamba hawaweiz kumpigia kura."

Kauli hiyo ya Cohen imekuja baada ya Bi. Omarosa Manigault Newman, Mmarekani mwenye asili ya Afrika aliyefanya kazi miezi kadhaa katika Ikulu ya White House kuandika katika kitabu chake kuwa Trump ni mbaguzi wa rangi. Amesema Trump alikuwa akiwatusi watu weusi mara kwa mara kabla ya kuwa rais wakati wa kutayarisha kipindi chake cha televisheni cha The Apprentice.

Cohen anasema Trump aliendelea kuwatusi watu weusi kwa kusema: "Nitajie nchi moja ambayo inatawaliwa na mtu mweusi ambayo si shimo la kinyesi."

 Michael Cohen

Kauli hiyo ya Cohen inaonekana kuthibitisha habari kuwa Trump alinukuliwa mwaka huu katika kikao cha faragha ndani ya White House akisema Haiti na baadhi ya mataifa ya Afrika ni nchi ambazo ni 'shimo la kinyesi'.