Mashirika ya Ulaya yapinga ombi la Marekani la kususia Huawei
Mashirika makubwa ya mawasiliano brani Ulaya yamepinga ombi la Marekani la kulisusia shirika kubwa la mawasiliano la China, Huawei.
Mashirika ya Ulaya yametupilia mbali madai kuwa shirika la Huawei hutumia vifaa vyake vya kielektroniki kufanya ujasusi kwa niaba ya serikali ya China.
Madai hayo yalitolewa dhidi ya shirika hilo la China baada ya shirika la ujasusi la Poland kumkamata Wang Weigin, mfanyakazi wa Huawei, pamoja na afisa wa zamani wa usalama Poland mnamo Januari 8.
Nchi zinazodai kuwa Huawei inafanya ujasusi hazijaweza kutoa ushahidi wowote na shirika la Huawei binafsi linakanusha tuhuma hizo. Nchi kadhaa za Ulaya, chini ya mashinikizo ya Marekani zimeanza kuiwekea Huawei vizingiti.
Gazeti la Ujerumani la Der Spiege, limeandika kuwa serikali ya nchi hiyo iko chini ya mashinikizo ya Marekani ya kususia Huawei. Shirika la Mawasiliano la Ujerumani, Deutsche Telekom limepuuzilia mbali madai ya Marekani na kutangaza mapatano na Huawei kuhusu mtandao wake wa 5G nchini Poland.
Disemba Mosi pia Disemba Mosi kufuatia ombi la Marekani, Bi. Meng Wanzhou Mkurugenzi wa Masuala ya Fedha katika shirika la Huawei, alikamatwa wakati akiwa katika uwanja wa ndege mjini Vancouver, Canada. Wanzhou aliachiliwa huru kwa dhamana baada ya serikali ya China kuionya Canada lakini kesi yake ingali inaendelea.
Kushinikizwa shirika la Huawei kunatajwa kuwa ni sehemu ya vita vya kibiashara kati ya China na Marekani kutokana na bidhaa za teknolojia za China kutia fora duniani kutokana na ubora pamoja na bei nafuu.