Moscow yatahadharisha kuhusu tuhuma za kuingilia uchaguzi wa Marekani mwaka 2020
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amewaambia wabunge wa Marekani kwamba Moscow inapinga uingiliaji kati wowote katika uchaguzi ujao wa Rais wa Marekani.
Sergei Ryabakov amewatahadharisha wabunge wa Marekani na kueleza kuwa tuhuma za kukaririwa dhidi ya Moscow kuhusu kuingilia kati uchaguzi wa rais wa Marekani zinasabababisha madhara makubwa katika uhusiano wa pande mbili. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameongeza kuwa, uhusiano kati ya Marekani na Russia haujaboreka.
Ryabakov amesema kuwa Marekani ineingia katika kipindi cha kampeni za uchaguzi na kampeni hizo zinapamba moto; hivyo na kwa kutilia maanani hisia za chuki dhidii ya Moscow baina ya aghlabu ya viongozi wa Marekani hususan ndani ya serikali ya nchi hiyo ni vigumu kuweza kumtayarisha rais ajaye uwanja mzuri wa kuainisha majukumu mbalimbali.
Sergei Ryabakov ametaja madai yanayosema kwamba Russia iliingilia kati uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka 2016 kuwa hayana msingi. Ikulu ya rais wa Russia (Kremlin) imepinga mara kadhaa madai hayo.