Mtaalamu wa uchumi Islamabad: Mafuta ya Iran yamesaidia ustawi wa Pakistan
https://parstoday.ir/sw/news/world-i57701-mtaalamu_wa_uchumi_islamabad_mafuta_ya_iran_yamesaidia_ustawi_wa_pakistan
Mtaalamu wa masuala ya kiuchumi wa nchini Pakistan amesema kuwa, kuongezeka uagizaji mafuta kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Kiislamu ya Iran kunakofanywa na serikali ya Islamabad mbali na kwamba kumesaidia kukidhi mahitaji ya nishati hiyo muhimu kwa taifa hilo, lakini pia ni hatua kubwa kwa ajili ya ustawi wa kiuchumi wa Pakistan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 05, 2019 23:21 UTC
  • Mtaalamu wa uchumi Islamabad: Mafuta ya Iran yamesaidia ustawi wa Pakistan

Mtaalamu wa masuala ya kiuchumi wa nchini Pakistan amesema kuwa, kuongezeka uagizaji mafuta kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Kiislamu ya Iran kunakofanywa na serikali ya Islamabad mbali na kwamba kumesaidia kukidhi mahitaji ya nishati hiyo muhimu kwa taifa hilo, lakini pia ni hatua kubwa kwa ajili ya ustawi wa kiuchumi wa Pakistan.

Rahmatullah Khan Wardak ameyasema hayo katika mahojiano na jarida la kila wiki la Nidai Millat na kubainisha kwamba mabadilishano ya mafuta kati ya Iran na pia hatua ya kuzuia magendo ya mafuta ya nchi hiyo, sambamba na kudhamini mahitaji ya Pakistan, kadhalika yameweza kusaidia ustawi wa mashirika ya mafuta nchini humo. Aidha Wardak ameongeza kwamba mabadilishano hayo yatasaidia hata kudhamini uchumi wa Pakistan. 

Viongozi wa Iran na Pakistan wakipeana mkuno wa ishara ya uhusiano wao mwema 

Mtaalamu huyo wa masuala ya kiuchumi wa nchini Pakistan sambamba na kubainisha kuwa biashara ya moja kwa moja na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kwa maslahi ya nchi hiyo amesema kuwa, mapato ya uagizaji mafuta kutoka Iran yanadhamini moja kwa moja nakisi ya kifedha ya serikali kama ambavyo yanaiwezesha nchi hiyo kupambana na matatizo yake ya kiuchumi. Rahmatullah Khan Wardak ameitaka serikali ya Islamabad kupuuza vikwazo vya upande mmoja vya Marekani na ugaidi wake wa kiuchumi na badala yake iongeze kiwango cha urafiki na ujirani mwema na Iran kwa ajili ya maslahi makuu ya kitaifa na kwamba vikwazo hivyo vya Washington mbali na Iran pia vinaidhuru Pakistan na eneo kwa ujumla.