Sisitizo la Abdullah Abdullah la kuunda serikali pana huko Afghanistan
https://parstoday.ir/sw/news/world-i60312-sisitizo_la_abdullah_abdullah_la_kuunda_serikali_pana_huko_afghanistan
Abdullah Abdullah ambaye anajitambua kuwa ndiye Rais wa Afghanistan amesema kuwa atatangaza baraza la mawaziri iwapo mpango wa kuunda serikali ya mirengo yote nchini humo hautakubaliwa.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Apr 11, 2020 23:51 UTC
  • Sisitizo la Abdullah Abdullah la kuunda serikali pana huko Afghanistan

Abdullah Abdullah ambaye anajitambua kuwa ndiye Rais wa Afghanistan amesema kuwa atatangaza baraza la mawaziri iwapo mpango wa kuunda serikali ya mirengo yote nchini humo hautakubaliwa.

Abdullah Abdullah ambaye amerefusha muda wa kufanya mazungumzo na Rais Muhammad Ashraf-Ghani wa Afghanistan ili kufikia mapatano ya kisiasa kufuatia ombi la viongozi wa kisiasa wa nchi hiyo ametahadharisha kuwa atatoa dikrii kuu ya serikali iwapo mpango wa serikali pana hautaafikiwa nchini humo. 

Fadhil Ahmad Maanawi mmoja wa wajumbe wa ngazi ya juu wa timu ya utulivu na utengamano katika uchaguzi wa Rais wa Afghanistan chini ya uongozi wa Abdullah Abdullah pia ametangaza kuwa hadi sasa hakujafikiwa mapatano yoyote wala hakuna hatua zilizopigwa kati yao na Muhammad Ashraf-Ghani; na kila upande unaendelea kushikilia misimamo yake.

Rais Ashraf-Ghani wa Afghanistan 

Kwa mujibu wa mpango wa Abdullah Abdullah wa kuanzishwa serikali itakayojumuisha pande kadhaa; timu mbili zilizoongoza katika uchaguzi zinapasa kuunda serikali hiyo. Aidha timu moja inapaswa kufanya kazi katika muundo ujao wa kisiasa wa Afghanistan kama Rais wa nchi na nyingine kama Waziri Mkuu. Mpango huo wa kuunda serikali pana uliopendekezwa  na Abdullah Abdullah ili kuiondoa Afghanistan katika mgogoro wa uchaguzi ni wa mfano ambao Abdallah aliukusudia katika serikali ya zamani ya nchi hiyo kati ya miaka ya 2014 hadi 2019 kwa mujibu wa vioengee vya makubaliano ya kisiasa ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa hata hivyo hakuweza kuutekeleza.  

Baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi uliozusha makelele mengi wa duru ya nne ya uchaguzi wa Rais wa Afghanistan uliofanyika Septemba iliyopita na kuzusha mambo sawa na yale yaliyoshuhudiwa baada ya uchaguzi wa kabla yake wa mwaka 2014 matokeo ambayo yalimpelekea Abdullah kutoa pendekezo la kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ili kusitisha mivutano ya kiuchaguzi kati yake na Ashraf-Ghani.  

Licha ya kuwa katika mpango huo wa uundaji serikali ya umoja wa kitaifa uliungwa mkono na kutilia mkazo suala la mgawo wa asilimia 50 kwa Abdullah na Ashraf-Ghani katika suala la madaraka lakini kutowekwa wazi jambo hilo kuliwafanya wawili hao kuyatazama mapatano hayo kwa hali mahsusi. Hata kama Ashraf-Ghani alikuwa ameahidi kuunda baraza la mashauriano ya amani la Loya Jirga na kuifanyia marekebisho katiba, kuanzisha cheo cha Waziri Mkuu na kiti hicho kukaliwa na Abdullah miaka miwili baada ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa mwaka 2016 lakini ahadi hiyo haikutekelezwa.  

Baraza la mashauriano ya amani la Afghanistan- Loya Jirga 

Kwa kuzingatia uzoefu mchungu aliopata Abdullah Abdullah katika kuunda serikali jumuishi baina yake na Ashraf-Ghani katika miaka mitano iliyopita na kutopewa asilimia sawa katika masuala ya uongozi wa nchi, kulisababisha kujitenga na Abdullah na baadhi ya wanasiasa na kutoka ndani ya chama; haya yote mara hii yamemfanya azingatie na kutilia maanani changamoto za duru iliyopita na hivyo kufanya kila awezalo ili kuweka wazi kikamilifu mgawo wake na Ashraf-Ghani katika mpango wa kuunda serikali pana huko Afghanistan. 

Mpango huo ambao baadhi ya vyombo vya habari vya Afghanistan vimeudokeza unaeleza kuwa Rais anapasa kuwa na mgawo wa asilimia 40 wa kuainisha mawaziri na viongozi wa kieneo hata hivyo Waziri Mkuu ana mgawo wa asilimia 60 katika uwanja huo. Kwa kuzingatia mgawo huo wa asilimia 40 na 60 katika mpango huo ambao umempatia Abdullah uhalali zaidi katika nafasi ya Waziri Mkuu ili kuwafuta kazi na kuwateuwa viongozi wa kitaifa na wa kieneo, ni jambo lililo mbali kwa Ashraf-Ghani kuweza kiurahisi kuafiki hali hiyo ya mambo. 

Hasa ikizingatiwa kuwa mpango wa serikali jumuishi unadhoofisha mfumo wa Urais wa Afghanistan kwa kuwa umezingatia asilimia 40 apatiwe Rais katika kuwateuwa viongozi wa kitaifa na kieneo; na Ashraf-Ghani anaweza kuupinga mpango huo kwa kisingizio kuwa mpango huo unakinzana na katiba ya nchi hiyo na hivyo kumfanya Abdullah akabiliwe na changamoto nyingi kutoka kwa fikra za walio wengi.