Joe Biden amtangulia Rais Donald Trump katika uchunguzi wa maoni
https://parstoday.ir/sw/news/world-i60341-joe_biden_amtangulia_rais_donald_trump_katika_uchunguzi_wa_maoni
Televisheni ya CNN nchini Marekani imetangaza kwamba, Joe Biden, mwakilishi wa chama cha Democrat katika uchaguzi wa rais nchini humo anamtangulia Rais Donald Trump katika uchunguzi wa maoni ya Wamarekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 13, 2020 03:27 UTC
  • Joe Biden amtangulia Rais Donald Trump katika uchunguzi wa maoni

Televisheni ya CNN nchini Marekani imetangaza kwamba, Joe Biden, mwakilishi wa chama cha Democrat katika uchaguzi wa rais nchini humo anamtangulia Rais Donald Trump katika uchunguzi wa maoni ya Wamarekani.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni, Biden amemtangulia Trump. Kutokana na matokeo hayo, wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, baada ya Bernie Sanders, aliyekuwa mmoja wa wagombea wa Democrat kwa ajili ya uchaguzi wa rais mwaka huu nchini Marekani, kujiengua katika mchakato wa kuwania tiketi ya chama hicho, Biden ameonekana kumtangulia Trump. Bernie Sanders alitangaza kuachana na mchuano wa kuwania tiketi ya chama cha Democratic kwa ajili ya uchaguzi wa 2020 siku ya Jumatano iliyopita.

Donald Trump na Joe Biden

Baada ya kutangazwa habari hiyo, Trump ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter akiwataka wafuasi wa Sanders kujiunga na chama chake cha Republican. Hii ni katika hali ambayo katika uchaguzi wa hivi karibuni wa ndani ya chama cha Democrat katika jimbo la Alaska, Biden aliibuka mshindi. Uchaguzi wa rais nchini Marekani utafanyika mwezi Novemba mwaka huu ambapo inatazamiwa kuwa Trump atachuana na hasimu wake mkubwa wa kisiasa, Joe Biden.