Afghanistan yazitaka nchi za Kiislamu kulaani jinai za Wazayuni
https://parstoday.ir/sw/news/world-i61141-afghanistan_yazitaka_nchi_za_kiislamu_kulaani_jinai_za_wazayuni
Baraza la 'Ikhwatul-Muslimin' katika jimbo la Balkh nchini Afghanistan limewataka viongozi wa nchi za Kiislamu na Kiarabu kuhitimisha kimya chao dhidi ya jinai zinazotendwa na utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya taifa madhlumu la Palestina.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 22, 2020 11:08 UTC
  • Afghanistan yazitaka nchi za Kiislamu kulaani jinai za Wazayuni

Baraza la 'Ikhwatul-Muslimin' katika jimbo la Balkh nchini Afghanistan limewataka viongozi wa nchi za Kiislamu na Kiarabu kuhitimisha kimya chao dhidi ya jinai zinazotendwa na utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya taifa madhlumu la Palestina.

Baraza hilo limebainisha kwamba Quds na Baitul-Muqaddas ni mali ya Waislamu wote duniani na kwamba Marekani na Wazayuni zinawanyima raia madhlumu wa Palestina ambao ni sehemu ya umma wa Kiislamu, haki zote za kibinaadamu na Kiislamu. Aidha baraza hilo lenye makao yake katika jimbo la Balkh nchini Afghanistan sambamba na kupongeza uvumbuzi wa Imam Khomeini (MA) Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kuitaja Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds, limezitaka asasi za kimataifa za kutetea haki za binaadamu na viongozi wa nchi za Kiislamu kutekeleza majukumu yao ya kibinaadamu na Kiislamu hususan ya kutonyamazia kimya mpango wa fedheha wa 'Muamala wa Karne' na badala yake watetee haki halali za Waislamu wa Palestina.

Bendera za taifa madhlumu la Palestina

Aidha Baraza la 'Ikhwatul-Muslimin' katika jimbo la Balkh nchini Afghanistan limeutaka Umoja wa Mataifa kutoa tamko kali la kulaani mwendelezo wa uvamizi wa utawala bandia wa Kizayuni dhidi ya ardhi za Palestina na kitendo cha utawala huo cha kuendelea kuidhibiti Quds na ujitenge na vitendo vya utawala huo.