Waziri wa Ulinzi wa China aitahadharisha Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i61274-waziri_wa_ulinzi_wa_china_aitahadharisha_marekani
Waziri wa Ulinzi wa China amesema kuwa ushindani wa nchi hiyo na Marekani umeingia katika nukta nyeti na hatari na kwamba China ni lazima iimarishe zaidi moyo wa kusimama imara.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 28, 2020 21:52 UTC
  • Waziri wa Ulinzi wa China aitahadharisha Marekani

Waziri wa Ulinzi wa China amesema kuwa ushindani wa nchi hiyo na Marekani umeingia katika nukta nyeti na hatari na kwamba China ni lazima iimarishe zaidi moyo wa kusimama imara.

Wei Fenghe ameyasema hayo kando ya kikao cha Kongresi ya Kitaifa ya Watu wa China mjini Beijing na kuchukua hatua ambayo si ya kawaida ya kuitaja kwa jina moja kwa moja Marekani kuhusiana na suala hilo na kuongeza kuwa, ni lazima kuimarishwa moyo wa mapambano na kusimama imara kwa ajili ya kuimarisha amani.

Wei Fenghe, Waziri wa Ulinzi wa China

Waziri wa Ulinzi wa China ameongeza kwamba, Marekani inaiwekea mashinikizo China kupitia tuhuma za kuenea virusi vya Corona sambamba na kuiwekea vizuizi vingi, na kwa ajili hiyo Beijing ni lazima iimarishe moyo wa mapambano. Wei Fenghe amesema hayo baada ya hotuba ya Rais Xi Jinping wa China aliyelitaka jeshi la nchi hiyo kujiweka tayari kwa ajili ya vita. Marekani imekuwa ikiingilia masuala ya ndani ya eneo la Taiwan na Hong Kong, suala ambalo limekuwa likikosolewa vikali na China.