Polisi ya Marekani yaendeleza mabavu dhidi ya waandishi habari
https://parstoday.ir/sw/news/world-i61331-polisi_ya_marekani_yaendeleza_mabavu_dhidi_ya_waandishi_habari
Wafanyakazi wawili wa shirika la habari la Reuters wamepigwa risasi wakati wakiwa kazini wakichukua picha kuhusu maandamano ya kulaani ubaguzi wa rangi na jinai ya polisi mweupe wa nchini Marekani ambaye hivi karibuni alimuua Mmarekani mwenye asili ya Afrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 31, 2020 23:17 UTC
  • Polisi ya Marekani yaendeleza mabavu dhidi ya waandishi habari

Wafanyakazi wawili wa shirika la habari la Reuters wamepigwa risasi wakati wakiwa kazini wakichukua picha kuhusu maandamano ya kulaani ubaguzi wa rangi na jinai ya polisi mweupe wa nchini Marekani ambaye hivi karibuni alimuua Mmarekani mwenye asili ya Afrika.

Picha iliyorekodiwa na mwandishi habari kwa jina la Julio-Cesar Chavez inamuonyesha polisi akimpiga risasi moja kwa moja mwandishi huyo wakati polisi wakiwatawanya wafanya maandamano. Aidha dakika kadhaa baadaye Chavez na Rodney Seward washauri wa shirika la habari la Reuters walijikuta wakipigwa risasi za plastiki wakati wakikimbia upande wa kituo cha mafuta kwa ajili ya hifadhi. 

Tukio hilo lilijiri huku watu hao wakitambulika waziwazi kama waandishi wa habari. 

Aidha Ijumaa iliyopita ripota mwingine wa televisheni katika jimbo la Kentucky alikabiliwa na risasi ya pilipili kutoka kwa polisi wa Marekani na kupelekea uongozi wa polisi wa jimbo hilo kuomba radhi.  

Miji mbalimbali nchini Marekani khususan mji wa Minneapolis katika jimbo la Minnesota imekumbwa na maandamano ya wananchi wanaolalamikia vikali vitendo vya ubaguzi wa rangi vya polisi. Itakumbukwa kuwa polisi katika mji wa Minneapolis majuzi ilimuua kikatili raia mwenye asili ya Afrika kwa jina la George Floyd na hivyo kuibua wimbi kubwa la maandamano na machafuko ya kupinga jinai hiyo. 

George Floyd alivyouliwa kikatili na polisi wa Marekani