Obama ataka kufanyiwa marekebisho mfumo wa kimahakama wa Marekani
Barack Obama, Rais wa zamani wa Marekani na katika kuendelea kwa maandamano ya kulaani mauaji ya ubaguzi wa rangi nchini humo, ametaka kufanyika mabadiliko katika mfumo wa vyombo vya mahakama vya nchi hiyo.
Obama ameyasema hayo kuhusiana na maandamano ya waandamanaji wanaopinga mauaji ya George Floyd, raia wa Marekani mwenye asili ya Afrika aliyeuawa wiki iliyopita na polisi mzungu na kuongeza kwamba: 'Zidisheni juhudi zenu kwenye chaguzi za kimajimbo na kieneo na muwashinikize viongozi husika katika ngazi hizo ili wapate kufanya marekebisho maalumuu kwenyye mfumo wa vyombo vya mahkama.' Rais huyo wa zamani wa Marekani ameongeza kwamba iwapo mwenendo huo utaendelea, basi Wamarekani wanaweza kuwa na matumaini ya kuwa na maisha bora yasiyokuwa na ubaguzi wa rangi nchini humo.
Rais wa zamani wa Marekani amesema tena kwamba, watu wanaotaka mabadiliko, ni lazima wasimame imara dhidi ya rais na viongozi wengine wa serikali kuu wanaoruhusu ufisadi na ubaguzi wa rangi nchini humo.