Askari wengi wa Marekani watangaza mshikamano wao na waandamanaji
https://parstoday.ir/sw/news/world-i61380-askari_wengi_wa_marekani_watangaza_mshikamano_wao_na_waandamanaji
Idadi kubwa ya polisi wa Marekani na kinyume na takwa la Rais Donald Trump la kuzidisha ukandamizaji dhidi ya waandamanaji, wametangaza mshikamano wao na waandamanaji.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 02, 2020 23:59 UTC
  • Askari wengi wa Marekani watangaza mshikamano wao na waandamanaji

Idadi kubwa ya polisi wa Marekani na kinyume na takwa la Rais Donald Trump la kuzidisha ukandamizaji dhidi ya waandamanaji, wametangaza mshikamano wao na waandamanaji.

Baadhi ya polisi wa nchi hiyo wameonekana wakiwakumbatia waandamanaji, wakiwaombea dua na kuwapa mkono wa pole kwa kupiga magoti mbele yao wakitoa heshima kwa George Floyd, Mmarekani mweusi aliyeuawa kinyama hivi karibuni na polisi mzungu. Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya CNN, askari polisi wengi katika mji wa Atlanta ulio jimbo la Georgia wameonekana wakishikana mikono na kupiga magoti mbele ya waandamanaji.

Polisi wakishirikiana na waandamanaji nchini Marekani

Hii ni katika hali ambayo Jumatatu iliyopita, Paul Pazen mkuu wa polisi katika jimbo la Colorado pia alionekana akiwa katika safu ya waandamanaji. Aidha Terence Monahan, mkuu wa idara ya polisi ya mji wa New York ameonekana akimkumbatia mmoja wa waandamanaji katika mji huo. Katika maandamano ya hivi karibuni nchini Marekani mamia ya watu wakiwemo waandishi wa habari, wamejeruhiwa na kutiwa mbaroni.