Seneta wa Kimarekani atahadharisha juu ya uwezekeno wa kusambaratika Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i61388-seneta_wa_kimarekani_atahadharisha_juu_ya_uwezekeno_wa_kusambaratika_marekani
Seneta wa chama cha Democrat nchini Marekani ametahadharisha kwamba kuendelea ubaguzi wa rangi nchini humo bila shaka kutaisambaratisha nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 03, 2020 03:29 UTC
  • Seneta wa Kimarekani atahadharisha juu ya uwezekeno wa kusambaratika Marekani

Seneta wa chama cha Democrat nchini Marekani ametahadharisha kwamba kuendelea ubaguzi wa rangi nchini humo bila shaka kutaisambaratisha nchi hiyo.

Chris Murphy ameyasema hayo kupitia ujumbe wa video alioutuma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na kusema kuwa, taifa la Marekani ni taifa lililofeli, ambalo halijaweza kufikiria kitu kingine kilicho bora zaidi kuliko rangi ya ngozi wala kufikiria kujenga jamii iliyosimama juu ya misingi ya usawa. Seneta huyo wa Marekani ameandika pia kwenye mtandao huo wa kijamii kwamba, maandamano ya amani ya mamilioni ya Wamarekani weusi ambao kwa miongo na karne kadhaa sasa wamekuwa wahanga wa unyanyasaji na ukandamizaji, hayajasaidia lolote katika kupunguza masaibu yao. Chris Murphy ameongeza kwamba, kuchaguliwa Donald Trump kuwa rais wa Marekani ni dhihirisho tosha la kushindwa na kufeli taifa la Marekani, kwa kuwa kumezidisha tu ubaguzi na kutaka kujitenga majimbo ya nchi hiyo. 

Chris Murphy, Seneta wa chama cha Democrat nchini Marekani

Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetoa taarifa ya kulaani kitendo cha polisi wa Marekani kuwalenga waandishi wa habari wa Shirika la Habari la Sputnik la Russia ambao walikuwa wanaakisi maandamano ya wananchi, na kukitaja kitendo hicho kuwa cha uhasama. Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia sambamba na kulaani kitendo hicho cha polisi wa mji wa Washington, imesisitiza kwamba Marekani inaendelea kukiuka ahadi zake hasa kuhusiana na kudhamini usalama wa waandishi wa habari. Taarifa hiyo ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, imezitaka taasisi za kimataifa pia kufuatilia matukio yanayoendelea hivi sasa Marekani. Hii ni katika hali ambayo James Slack, Msemaji wa Waziri Mkuu wa Uingereza pia sambamba na kuonyesha wasi wasi kutokana na ukatili wa maafisa wa polisi wa Marekani dhidi ya waandishi wa habari katika ghasia za kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo, amemtaka RaisTrump kutetea haki za waandishi wa habari.