Binti wa Donlad Trump ashutumiwa kwa kufanya utapeli
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Washington amesema kuwa, matamshi yaliyotolewa na Ivanka Trump, binti wa rais wa Marekani, Donald Trump akijaribu kumvua baba yake na tuhuma za fedha, ni ya kitapeli.
Mtandao wa habari wa The Hill umenukuu Karl Racine, Mwendesha Mashataka Mkuu wa Washington akisema kwamba, baada ya kumsaili Ivanka Trump kuhusu ubadhirifu wa fedha uliofanywa na baba yake wakati akiapishwa kuwa rais wa Marekani mwaka 2017 imegundulika kwamba ushahidi alioutoa ni wa kitapeli hasa kuhusiana na uchunguzi wa gharama zilizotumika kwenye sherehe hizo.
Ivanka Trump ambaye ni mshauri mkuu wa baba yake, Donald Trump, ameitwa katika Wizara ya Mahakama ya Marekani kwenda kutoa maelezo kuhusu fedha zilizotumika kugharamia sherehe za ushindi wa baba yake mwaka 2017.
Katika kesi hiyo iliyoanza kusikiliwa mwezi Januari mwaka huu wa 2020, rais wa Marekani Donald Trump, anatuhumiwa kutumia fedha vibaya kwa matumizi yake binafsi.
Mbali na Ivanka, mke wa Donald Trump, Melania Trump naye ameitwa kusailiwa kuhusiana na tuhuma hizo.
Trump na wafuasi wake wanakabiliwa na tuhuma nyingi ya ufisadi, ubadhirifu wa mali ya umma, kukwepa kulipa kodi, ufuska na tuhuma nyingine nyingi.
Maafisa wa Ikulu ya Marekan, White House wamefichua kuwa, huenda Donald Trump atatumia amri ya msamaha kwa wote, ili kuepusha kufungwa yeye na wafuasi wake kutokana na mashtaka mengi yanayowakabili.