'Waliohudumu White House katika utawala wa Trump huenda watapata tabu kuajiriwa'
https://parstoday.ir/sw/news/world-i65420-'waliohudumu_white_house_katika_utawala_wa_trump_huenda_watapata_tabu_kuajiriwa'
Gazeti la The Guardian linalochapishwa nchini Uingereza limeandika kuwa, wafanyakazi wa Ikulu ya White House katika kipindi cha utawala wa Donald Trump yamkini wakakabiliwa na tatizo la kupata ajira.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 26, 2020 23:07 UTC
  • 'Waliohudumu White House katika utawala wa Trump huenda watapata tabu kuajiriwa'

Gazeti la The Guardian linalochapishwa nchini Uingereza limeandika kuwa, wafanyakazi wa Ikulu ya White House katika kipindi cha utawala wa Donald Trump yamkini wakakabiliwa na tatizo la kupata ajira.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, wakati kila mara rekodi ya kufanya kazi katika Ikulu ya White House huwa ni fursa ya upendeleo kwa ajili ya kupata ajira mpya, rekodi ya utumishi kwa wale waliohudumu katika kipindi cha urais wa Trump, huenda ikawasababishia matatizo ya kupata ajira mpya baada ya kuondoka katika ikulu hiyo ya rais wa Marekani.

Guardian limebainisha kuwa, ukubwa wa doa la kufanya kazi katika kipindi cha urais wa Trump utachafua fursa za kupata  ajira katika siku za usoni kwa wafanyakazi wa White House wa wakati wa utawala wake na kwamba hali hiyo itakuwa ngumu zaidi kwa watu kama binti ya Trump, Ivanka na mume wake Jared Kushner ambaye ni mshauri mwandamizi wa rais huyo.

Kutoka kulia: Jared Kushner na Ivanka Trump katika kikao cha White House

Rais huyo wa Marekani anayemaliza muda wake, amevuruga mambo na kusababisha mifarakano ndani ya nchi hiyo, kiasi kwamba mjumbe mmoja mwandamizi wa masuala ya mitalaa ya uongozi katika Taasisi ya Brookings ya mjini Washington amesema, urais wa Trump haukuwa wa kawaida, kwa hivyo kipindi cha maisha yake ya baada ya urais pia hakitakuwa cha kawaida.

Wanasiasa wengi nchini Marekani wameukosoa utendaji wa Donald Trump katika kipindi cha miaka minne ya urais wake.../