Palestine Action yavamia kiwanda cha kuzalisha silaha cha Israel nchini Uingereza
https://parstoday.ir/sw/news/world-i73844-palestine_action_yavamia_kiwanda_cha_kuzalisha_silaha_cha_israel_nchini_uingereza
Kama sehemu ya kampeni yao ya kitaifa dhidi ya kiwanda kinachotengeneza silaha za Israeli, wanaharakati wanaounga mkono Palestina nchini Uingereza wamefanya maandamano nje ya kiwanda cha kampuni hiyo kwenye eneo Oldham na kuvamia paa la kiwanda hicho.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 23, 2021 12:50 UTC
  • Palestine Action yavamia kiwanda cha kuzalisha silaha cha Israel nchini Uingereza

Kama sehemu ya kampeni yao ya kitaifa dhidi ya kiwanda kinachotengeneza silaha za Israeli, wanaharakati wanaounga mkono Palestina nchini Uingereza wamefanya maandamano nje ya kiwanda cha kampuni hiyo kwenye eneo Oldham na kuvamia paa la kiwanda hicho.

Kundi la Palestine Action linalowatetea Wapalestina lenye makao makuu London huko Uingereza, limetangaza kuwa wanaharakati wake wamevamia paa la kiwanda cha silaha cha Israeli hii leo Jumatatu, wakiwa wameshikilia mabango yenye ujumbe 'Zima Elbit'.

Vilevile wanachama wa kundi hilo walifunga milango ya kiwanda cha silaha cha Israeli huko Oldham na kusimamisha uzalisha wa silaha katika kiwanda hicho.

Wanachama wa kundi hilo wamesisitiza kuwa wataendelea kuchukua hatua za kupiga vita kiwanda cha uzalishaji silaha za Israel cha Elbit ili kuvunja uhusiano wake na utawala katili wa Israeli licha ya jitihada za kuwafunga minyororo.

Wanaharakati wa Palestine Action

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye wavuti wake, Palestina Action imesema hatua hiyo inakuja wakati Israeli ikiendelea kushambulia jamii za Wapalestina huko Gaza na Ukingo wa Magharibi na kufanya unyama dhidi ya raia, ikitumia teknolojia na silaha ilizotengenezwa na Uingereza zinazozalishwa na kampuni kama Elbit Systems.

Taarifa hiyo imesema kiwanda cha silaha cha Oldham kinatumika kwa ajili ya kuzalisha teknolojia, aina mbalimbali za silaha, pamoja na vifaa vya ndege zisizo na rubani na vifaru vya vita vya Israel.

Hii nii mara ya pili katika miezi mitatu wanaharakati wanaounga mkono Wapalestina nchini Uingereza kuvamia paa la kiwanda cha silaha cha Israeli nchini humo.