Mar 22, 2022 12:53 UTC
  • Ripoti ya Chuo Kikuu cha Harvard yalaani uvamizi na uhalifu wa ubaguzi wa rangi wa Israel huko Palestina

Ripoti ya Kituo cha Haki za Binadamu cha Harvard imeibua hasira miongoni mwa maafisa wa utawala haramu wa Israel na duru zinazoiunga mkono Tel Aviv, baada kulaani uvamizi wa utawala huo huko Palestina ikiutaja kuwa ni "uhalifu wa ubaguzi wa rangi, apartheid."

Ripoti hiyo ya imetolewa sambamba na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ubaguzi wa Rangi, ambayo wanaharakati wameihuisha mjini London kwa kuupa jina jipya mtaa wa Ubalozi wa Israel.

Ripoti hiyo ilitolewa mwishoni mwa Februari na Kituo cha Haki za Kibinadamu katika Chuo cha Sheria cha Harvard kwa ushirikiano na Tasisi ya Palestina ya Dhamiri, na kisha kuwasilishwa katika Umoja wa Mataifa mapema mwezi huu wa Machi.

Kama ilivyo kawaida, umwakilishi wa Israel katika Umoja wa Mataifa, Gilad Erdan, ameeleza kukasirishwa kwake na ripoti hiyo akidai inawafanyia uadui Mayahudi na kukishutumu Chuo Kikuu cha Harvard kwamba kinashirikiana na taasisi za kigaidi dhidi ya Israeli!

Kwa upande mwingine, Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Marekani (CAIR) limepongeza ripoti ya Harvard na kusema, haiwezekani tena kukana na kuficha ukweli. Taarifa ya CAIR imehoji kwamba, lini jamii ya kimataifa itachukua hatua ya kukabiliana na uhalifu huu?

Ripoti ya Harvard imekuja baada ya ile ya Amnesty International mapema mwezi Februari, ambayo ilitangaza kwa mara ya kwanza kuwa Israel inatekeleza ubaguzi wa apartheid dhidi ya Wapalestina. 

Ripoti ya Amnesty International iliutuhumu utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni utawala wa baguzi wa rangi wa apartheid na kuwa taasisi ya karibuni zaidi ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu kuitangaza Israel kuwa ni utawala wa apartheid.

Ripoti yenye karibu kurasa 300 ya Amnesty International iliyopewa anwani "Mfumo wa Israel wa kutawala kikatili na kawandamiza Wapalestina" iliyotolewa Jumanne ya jana inaeleza vitendo vya kinyama vya kuwalazimisha watu kuondoka katika makazi yao, kuwekwa kizuizini, mauaji ya kikatili na majeraha makubwa, kunyimwa haki za msingi na kuwakandamiza na kuwatesa Wapalestina, na kuonesha jinsi utawala huo ulivyoundwa kwa msingi wa dhulma na ukandamizaji wa kimfumo dhidi yaWapalestina.

Awali mashirika ya Human Rights Watch na Israel B'Tselem yalikuwa yamesema, katika ripoti mbili tofauti kwamba Israel inatenda uhalifu wa ubaguzi wa rangi.

Tags