Papa Francis awaonya makasisi kuhusu hatari ya kutazama picha za ngono (ponografia)
(last modified Thu, 27 Oct 2022 13:16:35 GMT )
Oct 27, 2022 13:16 UTC
  • Papa Francis
    Papa Francis

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, amewaonya makasisi na watawa kuhusu hatari ya kutazama video au picha za ngono (ponografia) mtandaoni akisema "kunadhoofisha moyo wa kipadre".

Papa mwenye umri wa miaka 86, alikuwa akijibu swali kuhusu jinsi vyombo vya habari vya kidijitali na kijamii vinapaswa kutumiwa vyema, katika kikao kilichofanyika Vatican.

Anesema, watu wengi wana "tabia ya kutazama picha za ngono (ponografia) hata makasisi na watawa" na kwamba Ibilisi huingia kutokea huko.

Papa Francis ambaye pia alizungumzia suala la kupatanisha sayansi na imani na jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii na ulimwengu wa kidijitali, amesema ni lazima vitumike lakini amewashauri wasipoteze muda mwingi kutumia vitu hivyo.

Papa Francis

Amewashauri makasisi na watawa "kufuta picha na video za ngono katika simu zao, ili wasipate majaribu ".

Tafiti zinaonesha kwamba kutazama ponografia kuna matokeo mabaya kwa afya ya mwili na roho ya mwanaadamu. Vilevile huongeza tatizo la msongo wa mawazo.