Russia: Udhibiti wa mashindano ya uundaji silaha duniani umetoweka
https://parstoday.ir/sw/news/world-i96548-russia_udhibiti_wa_mashindano_ya_uundaji_silaha_duniani_umetoweka
Balozi wa Russia mjini Washington amesema, udhibiti wa mashindano ya uundaji silaha duniani umetoweka.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 22, 2023 11:45 UTC
  • Russia: Udhibiti wa mashindano ya uundaji silaha duniani umetoweka

Balozi wa Russia mjini Washington amesema, udhibiti wa mashindano ya uundaji silaha duniani umetoweka.

Marekani ina historia ndefu ya kukiuka mikataba na makubaliano ya kimataifa.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, Anatoly Antonov amesema, toleo la huko nyuma la Mkataba wa START limepitwa na wakati na inapasa kuwepo na umakini wa kufuatilia uwezo wa nchi wanachama wa shirika la kijeshi la NATO kuhusiana na udhibiti wa mashindano ya uundaji silaha.

Antonov amesema, Marekani na washirika wake wanapigania kuimarisha uwezo wao wa makombora kwa lengo la kuwa na nguvu na sauti ya juu kimataifa dhidi ya Russia na China.

Ameongeza kuwa mashindano ya uundaji silaha (duniani) hayadhibitiki tena.

Marais wa wakati huo wa Marekani na Russia wakisaina mkataba wa START

Hivi karibuni balozi huyo wa Russia mjini Washington aliionya Marekani kuwa Moscow na Washington hazitaweza kudumisha mawasiliano yao katika muktadha wa mkataba wao wa mwisho uliosalia wa silaha za nyuklia, ikiwa serikali ya Joe Biden haitabadilisha muelekeo wake juu ya uhusiano wa pande mbili.

Antonov aliongezea kwa kusema: "Marekani inatumia mantiki tatanishi. Kwa upande mmoja, wanaepuka kuamiliana nasi kwa ajili ya biashara za kawaida, na kwa upande mwingine, wanasisitiza kurejea kwenye ushirikiano wa kawaida juu ya suala la mkataba wa ukaguzi (wa silaha za nyuklia)".

Amesisitiza kuwa Moscow haikubaliani na mtazamo huo na kwamba kuwepo uhusiano mbaya kati ya Russia na Marekani kunaathiri udhibiti wa silaha.

Itakumbukwa kuwa mwaka 2003, Marekani ilichukua hatua ya upande mmoja ya kufuta mkataba wa makombora ya balestiki uliosainiwa kati ya Umoja wa Kisovieti, USSR na Marekani mnamo mwaka 2019, na ikajitoa pia katika mkataba wa kutokomeza makombora ya nyuklia ya masafa ya kati (INF), hatua ambayo ilithibitishwa na taarifa rasmi iliyotolewa na serikali ya Washington.../