May 09, 2023 10:42 UTC

Rais wa Russia ametangaza kwamba ustaarabu wa dunia unakabiliwa na mabadiliko makubwa, na kwamba lengo la Magharibi katika kueneza propaganda chafu dhidi ya Russia ni kuigawa nchi hiyo.

Akihutubia gwaride lililofanyika kwa ajili ya kuadhimisha ushindi katika Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wanazi wa Ujerumani Rais wa Russia amesema amesema "lengo lao ni kuona nchi yetu inaporomoka na kusambaratika."

Rais Vladimir Putin amekosoa sera za nchi za Magharibi na kusema kuwa nchi hizo zimesahau jinsi Wanazi walivyoshindwa na sasa zinaongoza propaganda chafu dhidi ya Russia.

Putin ameongeza kuwa, lengo la propaganda chafu dhidi ya Russia (Russophobia) ni kuigawa nchi hiyo; na wasomi wa Magharibi wanaamini kuwa wao ni watu wa kipekee na wanapigana vita kwa ajili ya kulinda jambo hilo.

Rais wa Ruussia amesisitiza kuwa: "Ukraine imekuwa mateka na chombo kinachotumiwa na Magharibi."

Putin mara kwa mara mekuwa akiifananisha serikali ya Ukraine na Wanazi walioshindwa katika Vita vya Pili vya Dunia.

Amewashutumu viongozi wa Ukraine kuwa  ni Wanazi mamboleo.

Kuhusiana na lengo la Moscow katika vita vya Ukraine, Putin mesema: "Moscow inataka kuona mustakabali wa amani, uhuru na utulivu, na kwa upande wake, Russia haina watu maadui Magharibi na Mashariki."

Tags