Jul 21, 2016 06:03 UTC
  • Alkhamis, Julai 21, 2016

Leo ni Akhamisi tarehe 16 Shawwal 1437 Hijria sawa na 21 Julai, 2016.

Siku kama ya leo miaka 128 iliyopita John Boyd Dunlop raia wa Uingereza, alikuwa mvumbuzi wa kwanza wa gurudumu. Dunlop alifikia hatua ya kuvumbua gurudumu la magari baada ya kupita miaka kadhaa ya utafiti. Alifariki dunia mwaka 1921.

Siku kama ya leo miaka 62 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 21 Julai 1954 ulitiwa saini mwishoni mwa mkutano wa Geneva mkataba wa kuacha vita kati ya Ufaransa na Vietnam na kukomesha ukoloni wa Ufaransa huko India na China. Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya kuanguka ngome imara ya Wafaransa iliyojulikana kwa jina la Dien Bien Phu nchini Vietnam Mei mwaka 1954. Makubaliano ya mkutano wa kimataifa wa Geneva, yalihudhuriwa na wawakilishi wa ngazi za juu kutoka Ufaransa, Marekani, Uingereza, China, Vietnam na Urusi ya zamani. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, vikosi vya kigeni vilipaswa kuondoka Vietnam, lakini Marekani kinyume na makubaliano ya Geneva, iliamua kutuma majeshi katika eneo hilo kwa lengo la kuzuia kuungana maeneo mawili ya Vietnam ya kaskazini na kusini.

Na tarehe 31 Tir miaka 28 iliyopita siku nne tu baada ya Iran kulikubali azimio nambari 598 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, jeshi la Saddam Hussein, dikteta wa zamani wa Iraq lilifanya mashambulizi makubwa katika maeneo ya kusini mwa Iran. Azimio hilo ambalo lilikuwa limepasishwa yapata mwaka mmoja kabla lilisisitiza udharura wa kusitishwa vita, kutangazwa mvamizi na kumlazimisha kutoa fidia za hasara zilizosababishwa na vita hivyo, kurejeshwa mateka wa pande mbili na vilevile kurejea majeshi ya pande mbili katika mipaka ya kimataifa. Utawala wa kichokozi wa Saddam ambao licha ya kwamba ulikuwa umelikubali rasmi azimio hilo lakini ulianzisha mashambulizi makubwa katika maeneo ya Iran baada ya Tehran kutangaza kuwa imelikubali azimio hilo.   

 

Tags