Sep 17, 2016 06:00 UTC
  • Ijumaa, Septemba 16, 2016

Leo ni Ijumaa tarehe 14 Dhulhija 1437 Hijria sawa na Septemba 16, 2016.

Miaka 280 iliyopita katika siku kama ya leo, alifariki dunia Daniel Gabriel Fahrenheit mwanahesabati na mwanafizikia wa Kijerumani aliyevumbua kipimajoto yaani thermometer, akiwa na umri wa miaka 50. Fahrenheit alikuwa na fikra ya kubuni kifaa ambacho kingekuwa na uwezo wa kupima kiwango cha joto na mwaka 1724 mwanafizikia huyo Mjerumani akafanikiwa kutengeneza kipimajoto hicho. Kifaa hicho ambacho kimepewa jina la msomi huyo mwenyewe yaani Fahreinheit, bado kinatumika hadi leo.

Daniel Gabriel Fahrenheit

Miaka 85 iliyopita mwafaka na siku hii ya leo, aliuawa Omar al Mukhtar kiongozi wa taifa la Libya katika mapambano ya ukombozi dhidi ya wakoloni wa Italia. Omar Mukhtar aliyekuwa kiongozi wa kidini alizaliwa mwaka 1859. Mwaka 1895 alielekea Sudan na kushiriki katika harakati za kupambana na ukoloni wa Uingereza. Baada ya kushindwa kwa harakati hizo, Omar Mukhtar alirejea nchini Libya. Mwaka 1911 Wataliano waliivaia Libya kwa lengo la kuitawala nchi hiyo. Kiongozi huyo wa kidini aliwahimiza wapiganaji wa makabila ya Libya kusimama kidete na kupambana dhidi ya wavamizi wa Kitaliano na kuwasababishi hasara kuwa. Hata hivyo kwa kutumia askari wengi zaidi na silaha za kisasa wavamizi hao walimzingira Omar Mukhtar na wenzake na kumkamata na kisha wakamnyonga katika siku kama ya leo.

Omar Mukhtar

Miaka 77 iliyopita katika siku kama ya leo, alifariki dunia Ayatullah Fayyaz Zanjani fakihi na msomi mahiri wa elimu ya Usuul. Awali alisoma kwa baba yake na baadaye akahudhuria masomo kwa walimu mahiri wa zama hizo mjini Tehran kama Mirza Muhammad Hassan Ashtiyani na kuwa mahiri katika taaluma za fikihi, Usuul, mantiki na tafsiri. Mwanazuoni huyo alikuwa Marjaa Taqlidi wa Zanjani. Kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30 alikuwa mmoja wa walinganiaji wakubwa wa mafundisho ya Ahlul Bayt (sa).

Ayatullah Fayyaz Zanjani

Tarehe 16 Septemba miaka 77 iliyopita Warsaw mji mkuu wa Poland ulizingirwa na Wajerumani, katika mwezi wa kwanza wa Vita vya Pili vya Dunia. Mashambulio ya wanajeshi wa Kinazi wa Ujerumani huko Poland yalianza siku 15 kabla ya kuanza vita hivyo.

Mkuu wa Poland

Na miaka 38 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria Shamsia, dikteta wa zamni wa Iraq Saddam Hussein alifuta kwa upande mmoja makubaliano ya mipaka ya mwaka 1975 yaliyojulikana kwa jina la Mkataba wa Algeria kati yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kwa hatua hiyo Saddam alitayarisha mazingira ya kuvamia ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Siku hiyo, Saddam Hussein aliuchana mkataba huo wa Algeria kwa kuungwa mkono na madola ya kibeberu katika hotuba aliyoitoa kwa njia ya redio na televisheni. Mkataba huo wa mwaka 1975 wa Algeria yalikuwa makubaliano ya mwisho kati ya nchi hizo mbili kwa ajili ya kutatua hitilafu za mipaka. Siku kadhaa baadaye, Saddam Hussein alianzisha uvamizi wa miaka minane dhidi ya ardhi ya Iran kwa uchochezi wa nchi za Magharibi.

dikteta wa zamni wa Iraq Saddam Hussein

 

 

 

Tags