Jan 09, 2017 23:25 UTC
  • Jumanne, 10 Januari, 2017

Jumanne tarehe 11 Rabiuthani 1438 Hijria sawa na tarehe 10 Januari 2017.

Siku kama ya leo miaka 54 iliyopita, wataalamu wawili wa Uswisi walifanikiwa kutengeneza saa ya elekroniki. Wataalamu Solvil na Titus baada ya kupitisha miaka 12 ya juhudi kubwa, hatimaye walifanikiwa kutengeneza chombo hicho kwa kuweka vifaa kadhaa muhimu na makini. Aina hii ya saa ni makini mno na hufanya makosa machache sana ikilinganishwa na saa nyingine. 

Siku kama ya leo miaka 60 iliyopita aliaga dunia Ustadh Abulqassim Sahab, mmoja kati ya wasomi wakubwa wa elimu za fiqhi na jiografia na mtafiti mashuhuri wa Kiirani. Alizaliwa mwaka 1266 Hijria Shamsiya katika mji wa Tafresh nchini Iran. Abulqassim Sahab alijifunza fiqih na usul kwa maulamaa wa mji huo na mbali na kupata elimu hiyo alizungumza pia lugha za Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu na Kijerumani. Msomi huyo mkubwa wa Iran ameandika karibu vitabu 70 na miongoni mwa vitabu hivyo ni kile cha Historia ya Maisha ya Maimamu na Kamusi ya Wataalamu wa Masuala ya Mashariki.

ابوالقاسم سحاب

Tarehe 10 Januari 1920, Jumuiya ya Mataifa ilianza shughuli zake rasmi huko Geneva, Uswisi. Jumuiya hiyo, iliundwa baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia, kwa shabaha ya kuleta amani na usalama duniani. Awali nchi za Kiafrika na Urusi hazikujiunga na jumuiya hiyo, na nchi za Uingereza na Ufaransa zilitosheka kwa kuiunga mkono. Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, mnamo mwezi Aprili 1946, uliundwa Umoja wa Mataifa na kuchukua nafasi ya Jumuiya ya Mataifa, ingawa matatizo yaliyokuwa yakiikumba Jumuiya ya Mataifa ambayo yalipelekea kusambaratika kwake bado yanaendelea kuukumba Umoja wa Mataifa.

سازمان ملل متحد

Siku kama ya leo miaka 192 iliyopita yaani tarehe 10 Januari 1824, Joseph Aspdin mwanakemia wa Uingereza, alifanikiwa kutengeneza saruji na kwa utaratibu huo kukapatikana mabadiliko makubwa katika shughuli za ujenzi. Hatua hiyo ilitambuliwa kama tukio kubwa katika shughuli za kimaendeleo na ujenzi mpya wa nyumba. Joseph Aspdin ambaye alikuwa akifanya utafiti kwa miaka kadhaa ili kutengeneza mada ambayo ingesaidia kuimarisha msingi wa nyumba, hatimaye alifanikiwa kutengeneza saruji baada ya majaribio chungu nzima.

Siku kama ya leo miaka 830 iliyopita, alizawa mjini Mosul, moja ya miji mashuhuri ya Iraq, Ibn Khallekan (Ebn-e Xallakan), kadhi, mwanahistoria na mtaalamu wa fasihi wa Kiislamu. Akiwa kijana alisoma elimu za awali katika mji alikozaliwa na kisha kufanya safari mbalimbali na kukutana na kupata elimu kwa wataalamu wa fiqhi na wanahistoria wakubwa wa Kiislamu. Kwa muda mrefu Ibn Khallekan alikuwa kadhi mjini Damascus, Syria na akiwa mtaalamu katika elimu za historia, fasihi ya Kiarabu na mashairi. Msomi huyo mkubwa wa Kiislamu alifariki dunia mwezi wa Rajab mwaka 681 Hijiria na kuzikwa chini ya mlima Qasioun ulio Damascus ambako pia wamezikwa wasomi wengi. Miongoni mwa vitabu muhimu vya Ibn Khallekan ni Wafahyatul A'yaan. 

ابن خلکان

Siku kama ya leo miaka 1218 iliyopita, alifariki dunia Abu Ali Khayyat, mnajimu na mtaalamu wa hesabati wa Kiislamu. Abu Ali ni mmoja wa shakhsia aliyekuwa na nafasi kubwa wakati wake huku jina lake likiwekwa mstari wa mbele katika kitabu cha majina ya wasomi wakubwa na mashuhuri wa dunia. Msomi huyo ameandika vitabu vingi maarufu zaidi kikiwa ni kitabu cha 'Mawaalid' na 'Siyarul-A'amaal.' Vitabu vingi vya Abu Ali Khayyat vimetarjumiwa kwa lugha ya Kilatini.

Na siku kama ya leo miaka 5 iliyopita maajenti wa shirika la ujasusi la Israel MOSSAD walimuua shahidi mtaalamu wa nyuklia wa Iran Mustafa Ahmad Roshan. Msomi huyo aliwa wa nne wa nyuklia kuuawa shahidi kwa njia ya kigaidi.

Mustafa Ahmad Roshan alishambuliwa alipokuwa njia akielekea kazini na kuuawa yeye pamoja na dereva wake, Reza Qashqavi. Siku chache baadaye vibaraka waliomuua msomi hiyo wa nyuklia wa Iran walikamatwa na kutoa taarifa kamili kuhusu ushirikiano wao na shirika la ujasusi la Israel Mossad na jinsi walivyepewa mafunzo ya kufanya mauaji ya kigaidi dhidi ya wataalamu wa nyuklia wa Iran.