Aug 02, 2020 01:32 UTC
  • Jumapili, Pili Agosti, 2020

Leo ni Jumapili tarehe 12 Mfunguo Tatu Dhul-Hija 1441 Hijria mwafaka na tarehe Pili Agosti mwaka 2020 Miladia.

Siku kama ya leo miaka 98 iliyopita Alexander Graham mvumbuzi wa wasimu wa Kiscotland na Kimarekani aliaga dunia. Alizaliwa huko Scotland na baada ya kukumbwa na maradhi ya Kifua Kikuu (TB) akiwa pamoja na familia yake alielekea Canada na baadaye Marekani. Akiwa Marekani Graham Bell alianza kufanya kazi ya kuhamisha sauti ambapo baada ya kufahamiana na Thomas Watson akafuatilia kwa bidii zaidi suala la kufanya majaribio kuhusu sauti ambapo mwaka 1876 alifanikiwa kuvumbua simu.***

Alexander Graham

 

Katika siku kama ya leo miaka 86 iliyopita alifariki dunia Fidel Hindenburg Rais wa zamani wa Ujerumani na Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vya majeshi ya nchi hiyo wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia. Hindenburg alichaguliwa kuwa Rais wa Kwanza wa Ujerumani mwaka 1925. ***

Fidel Hindenburg akiwa na Adolph Hitler

 

Miaka 75 iliyopita katika siku kama ya leo, kongamano la Potsdam lilikamilisha kazi zake. Kongamano hilo la tatu na la mwisho la viongozi waitifaki walioshiriki katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, lilianza tarehe 17 mwezi Julai na kumalizika tarehe Pili Agosti 1945. Kongamano hilo lililofanyika katika mji wa Potsdam karibu na mji mkuu wa Ujerumani, Berlin lilihudhuriwa na Joseph Stalin, Harry S. Truman na Winston Churchill, marais wa wakati huo wa Urusi ya zamani, Marekani na Uingereza. ***

Kongamano la Potsdam

 

Katika siku kama ya leo miaka 37 iliyopita, Ayatullah Mirza Muhammad Baqir Ashtiyani alifariki dunia. Alimu huyo ni mjukuu wa Mirza Muhammad Hassan Ashtiyani mmoja wa viongozi wa Harakati ya Tumbaku nchini Iran. Alizaliwa mjini Tehran na baada ya kukamilisha masomo ya awali alielekea katika mji wa Najaf huko Iraq na kuhudhuria masomo ya maulama mashuhuri wa zama hizo kama Ayatullah Mirza Naini na Sayyid Abul Hassan Isfahani. Ayatullah Muhammad Baqir Ashtiyani ameacha athari nyingi za vitabu zenye thamani kubwa katika nyanja mbalimbali.***

Mirza Muhammad Hassan Ashtiyani

 

Na miaka 30 iliyopita katika siku kama ya leo, jeshi la Iraq liliishambulia na kuikalia nchi jirani ya Kuwait. Huo ulikuwa uvamizi wa pili wa Iraq kwa jirani zake baada ya ule wa Iran wa mwaka 1980. Utawala wa Saddam ulikuwa ukidai kwamba, ardhi ya Kuwait ni sehemu ya ardhi yake. Mashambulio ya Iraq dhidi ya Kuwait yalikabiliwa na radiamali kali ulimwenguni. Nchi nyingi duniani na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilaani uvamizi huo na kuvitaka vikosi vya Iraq kuondoka mara moja katika ardhi ya nchi hiyo. Nchi kadhaa zikiongozwa na Marekani zilituma vikosi vyao vya kijeshi katika Ghuba ya Uajemi ili kuviondoa vikosi vamizi vya Iraq kutoka katika ardhi ya Kuwait na kuhitimisha uvamizi huo Februari 28 mwaka 1991. ***

Uharibifu unaoonekana baada ya mashambulio ya jeshi la dikteta Saddam dhidi ya Kuwait