Mar 10, 2024 11:53 UTC
  •  Sierra Leone yapongeza msaada endelevu wa China kwa maendeleo ya miundombinu ya nchi hiyo

Rais Julius Maada Bio wa Sierra Leone amepongeza msaada endelevu wa China kwa nchi yake katika maendeleo ya miundombinu ya nchi hiyo. Rais Bio ameeleza haya katika mahojiano aliyofanyiwa alipokuwa katika ziara ya kiserikali nchini China.

Itakumbukwa kuwa Rais wa Sierra Leone alifanya ziara rasmi nchini China kuanzia Febrari 27 hadi Machi 2. Ziara hiyo ilikuwa ya pili kuwahi kuifanya huko China tangu aingie madarakani.

China na Sierra Leone zina uhusiano wa kidiplomasia kati yazo kwa miongo kadhaa sasa; ambapo chini ya fremu ya ushirikiano wa nchi mbili miradi mingi ya ujenzi wa reli na madaraja imetekelezwa kwa mafanikio huko Sierra Leone. 

Mfano wa wazi wa ujenzi wa madaraja uliofanywa na China huko Sierra Leone tunaweza kutaja daraja la pili la Juba lililopewa jina la  shujaa mkubwa wa Sierra Leone, Sendgbe Pieh. Daraja hilo lina urefu wa mita 81.8 na linapatikana   magharibi mwa Freetown, mji mkuu wa Sierra Leone. 

Daraja la Sendgbe Pieh jini Free Town, Sierra Leone 

Rais wa Sierra Leone ameishukuru China kwa kujenga daraja hilo na kusema linasaidia katika kudhamini usalama wa wananchi hasa wanawake na watoto wakati wa vipindi vya mvua. 

Aidha, kuna miradi mingine mingi inayofadhiliwa na China katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika ambayo sasa inadhihirika kuwa ushahidi wa urafiki wa kudumu kati ya nchi hizo mbili.

Tags