Serikali ya Niger yatangaza maadhimisho ya mapinduzi kuwa ni "Sikukuu ya Kitaifa"
-
Jenerali Tiani
Serikali ya kijeshi ya Niger imetangaza Julai 26 kuwa ni Sikukuu ya Kitaifa itakayokuwa ikiadhimishwa kila mwaka nchini humo kusherehekea matendo ya kizalendo ya watu wa Niger.
Tarehe 26 mwezi Julai ni siku ambayo kundi la wanajeshi huko Niger lilifanya mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Rais wa nchi hiyo Mohamed Bazoum. Bazoum bado anashikiliwa na kikosi cha wanajeshi kilichoongozwa na mkuu wa zamani wa Gadi ya Rais, Jenerali Abdourahamane Tiani.

Jenerali Tiani alisema wakati alipochukua madaraka kuwa mapinduzi hayo yalikuwa halali kutokana na kuzorota hali ya usalama wakati wa utawala wa Bazoum.
Kiongozi wa utawala wa kijeshi wa Niger amesema kuwa, tarehe 26 Julai kila mwaka itakuwa ikiadhimishwa kuenzi vitendo vya uzalendo wa hali ya juu vya wananchi wa Niger katika kuunga mkono mamlaka ya kujitawala na uhuru wao.