Chad yataka kutengwe bajeti ya kupambana na ugaidi Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i11461-chad_yataka_kutengwe_bajeti_ya_kupambana_na_ugaidi_afrika
Rais Idris Deby wa Chad ametoa wito kwa nchi za Afrika kuanzishwa mfuko maalumu kwa ajili ya kupambana na ugaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 18, 2016 00:13 UTC
  • Chad yataka kutengwe bajeti ya kupambana na ugaidi Afrika

Rais Idris Deby wa Chad ametoa wito kwa nchi za Afrika kuanzishwa mfuko maalumu kwa ajili ya kupambana na ugaidi.

Rais wa Chad alitoa wito huo jana katika mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika unaoendelea Kigali nchini Rwanda. Deby amewataka viongozi wa nchi hizo kulipa kipaumbele suala la kupambana na ugaidi.

Amesema suala la kuanzishwa mfuko wa kupambana na ugaidi lina umuhimu mkubwa na kwamba bajeti ya suala hilo inapaswa kudhaminiwa na nchi za Afrika na washirika wa Umoja wa Afrika (AU).

Rais wa Chad ameashiria ongezeko la vitisho vya ugaidi na misimamo mikali katika maeneo mbalimbali ya dunia ikiwemo Afrika na kusisitiza kuwa, kuna udharura wa kuwepo suhula na zana za kutosha za kukabiliana na tatizo hilo.

Suala la kupambana na ugaidi liko katika ajenda ya mkutano wa 27 wa viongozi wa Umoja wa Afrika. Mkutano huo wa siku mbili ulianza jana mjini Kigali ukihudhuriwa na viongozi wa nchi za bara hilo.