Viongozi wa Afrika wasisitiza ushirikiano katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
(last modified Thu, 16 Jan 2025 11:06:50 GMT )
Jan 16, 2025 11:06 UTC
  • Viongozi wa Afrika wasisitiza ushirikiano katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Viongozi wa nchi za Kiafrika wamesisitiza udharura wa kushirikiana nchi za bara hilo na kubuni tekolojia ya kukabiliana na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi ili kuhakikisha bara la Afrika linapata maendeleo endelevu.

Viongozi wa nchi za Afrika wameleza haya katika hotuba zao katika Wiki Endelevu ya Abu Dhabi 2025.

Wakuu na Marais wa nchi mbalimbali za Afrika wamesisitiza katika hutoba zao huko Abu Dhabi katika Umoja wa Falme za Kiarabu kuhusu udharura wa kudumisha ushirikiano kati ya mataifa ya Afrika ili kuzipatia ufumbuzi taathira za mabadiliko ya hali ya hewa na kukuza uchumi wa bara hilo kwa maendeleo endelevu ya watu wake. 

Rais Bola Ahmed Tinubu wa Nigeria amesema hakuna nchi inayoweza kupiga hatua katika ustawi endelevu ikiwa peke yake. "Mapabano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi yanahitaji ushirikiano wa nchi mbalimbali," amesema Rais wa Nigeria.

Akihutubia mkutano huo, Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni amesema uwekezaji barani Afrika utahakikisha upatikanaji wa soko linalokuwa na kwamba nchi yake itashirikiana na mataifa mengine kuyafanyia kazi  mapendekezo yaliyowasilishwa katika mkutano wa Abu Dhabi.

Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda 

Naye Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema: Dhamira ya kisiasa pekee haiwezi kushughulikia suala la mabadiliko ya hali ya hewa na maendeleo endelevu, na amewataka viongozi wa nchi kuziba pengo kati ya utashi wa kisiasa na hatua za kivitendo.