Waziri Mkuu wa Senegal aliyefutwa kazi achaguliwa kuwa Spika wa Bunge
-
Ousmane Sonko, Spika wa Bunge la Senagal
Waziri Mkuu wa zamani wa Senegal Ousmane Sonko jana alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge la nchi hiyo akimrithi El Malick Ndiaye, aliyejiuzulu siku ya Jumapili.
Akihutubia bungeni baada ya kuchaguliwa, Sonko ameahidi kutotumia nafasi yake mpya kufuatilia malalamiko yake binafsi.
"Sitalitumia Bunge hili, wala Naibu wangu yoyote kulipiza kisasa," amesema Sonko.
Sonko amesema anafahamu ukubwa wa majukumu yaliyo mbele yake lakini akasema kuwa ana imani na uwezo wake wa kuliongoza bunge. Ametaja uzoefu wake kama mbunge kwa miaka mitano, pamoja na majukumu yake ya awali kama Meya na Waziri mkuu.
Spika Mpya wa Bunge la Senegal pia Sonko pia amempongeza Waziri Mkuu mteule Ahmadou Al Amine Lo, akimtaja kama "mtu mwenye uwezo, mchapakazi na mwenye kujitolea." Amesema anamjua vyema Lo “kikamilifu” na kwamba walifanya kazi pamoja kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu.
Mkuu huyo wa chama cha PASTEF pia amemsifu mtangulizi wake, El Malick Ndiaye, kwa kuboresha Bunge la Kitaifa na kuimarisha diplomasia ya bunge.