Kiongozi wa waasi Sudan Kusini aelekea Afrika Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i17266-kiongozi_wa_waasi_sudan_kusini_aelekea_afrika_kusini
Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini ambaye alikimbilia Khartoum baada ya mapigano makali yaliyotokea katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba, Julai mwaka huu baina ya wafuasi wake na jeshi la serikali ya Rais Salva Kiir, ameondoka Sudan na kuelekea Afrika Kusini.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 12, 2016 12:24 UTC
  • Kiongozi wa waasi Sudan Kusini aelekea Afrika Kusini

Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini ambaye alikimbilia Khartoum baada ya mapigano makali yaliyotokea katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba, Julai mwaka huu baina ya wafuasi wake na jeshi la serikali ya Rais Salva Kiir, ameondoka Sudan na kuelekea Afrika Kusini.

Rick Machar amesema kuwa, anaelekea Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa afya yake na kwamba ataondoka nchini humo baada ya hapo. Hata hivyo Machar hakueleza ataelekea wapi baada ya Afrika Kusini. 

Rick Machar alikimbia mji mkuu wa Sudan Kusini baada ya kupamba moto mapigano baina ya wafuasi wake na jeshi la serikali Julai mwaka huu kwa madai kuwa alinusurika jaribio la kutaka kumuua. 

Mapigano ya ndani Sudan Kusini

Mapigano ya ndani nchini Sudan Kusini yalianza mwaka 2013 kati ya jeshi linalomuunga mkono Rais Salva Kiir na wanamgambo watiifu kwa aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo Riek Machar. Wakati huo Rais Salva Kiir alimtuhumu makamu wake kuwa alifanya jaribio la kuipindua serikali yake. 

Maelfu ya watu wameuawa na wengine zaidi ya milioni moja wameazimika kuwa wakimbizi kutokana na mapigano hayo.