Maadui wa ash-Shabab waondoka katika mji waliouteka Somalia
Wanachama wa kundi lenye mafungamano na genge la kigaidi la Daesh, wameondoka katika eneo waliloliteka hivi karibuni la Qandala kaskazini mashariki mwa Somalia.
Habari zaidi zinaarifu kuwa, wanachama wa kundi hilo wameondoka mjini humo, huko Puntland kaskazini mashariki mwa Somalia baada ya kulidhibiti kwa masaa kadhaa.
Abdiweli Adan, mmoja wa viongozi wa kikabila katika eneo hilo amenukuliwa akisema kuwa, watu wenye silaha asubuhi ya Alkhamis ya jana, waliondoka katika mji huo baada ya kuudhibiti kwa masaa machache.
Inaelezwa kuwa, kiongozi wa kundi hilo anaitwa Abdul-Qadir Mu'min, mwenye mahusiano ya karibu na genge la ukufurishaji la Daesh. Kudhibitiwa mji wa Qandala na magaidi hao, kulikuja baada ya kujiri mapigano makali, baina yao na askari wa serikali ya Somalia.
Hii ni katika hali ambayo mwezi Agosti mwaka huu Wizara ya Ulinzi ya Marekani, (Pentagon) ililiweka jina la mkuu wa kundi hilo katika orodha ya magaidi wanaotafutwa. Kundi hilo lina uhasama na genge la ash-Shababni licha ya kwamba yote mawili na makundi ya Kiwahabi.