SAUTI, Watanzania: Kuchaguliwa Trump kumebainisha kuwa Wamarekani wote wana ubaguzi mioyoni mwao
Watanzania walio wengi wameonyesha masikitiko yao kufuatia ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa rais nchini Marekani kutokana na kile wanachokidai kuwa ni misimamo hasi ya kibaguzi ambayo mara nyingi alikuwa akiitoa katika kipindi chote cha kampeni.
Kwa mujibu wa Watanzania, kitendo cha Wamarekani kumchagua mtu huyo, kinabainisha wazi taswira halisi ya kibaguzi waliyonayo Wamarekani na kwamba misimamo ya rais huyo mteule ndio iliyomo mioyoni mwa raia wote wa taifa hilo linalojinadi kuwa mtetezi wa haki za binaadamu.
Kati ya matamshi ya kibaguzi na chuki aliyoyatoa Trump kipindi cha kampeni ni kuwafukuza Wafrika, kuwazuia Waislamu kuingia nchi hiyo, kujenga ukuta wa kibaguzi dhidi ya raia wa Mexico kuingia Marekani na mambo mengi kama hayo. Hayo yanajiri katika hali ambayo hadi sasa maandamano yameendelea kushuhudiwa katika miji mbalimbali nchini Marekani kupinga ushindi wa Trump. Waandamanaji hao ambao wamejawa na hasira wametangaza kutomtambua mtu huyo kama rais wao.
Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Dar es Salaam Omar Manji kwa taarifa kamili…../