Dec 10, 2016 03:56 UTC
  • Makumi wauawa katika mashambulizi ya kigaidi Nigeria

Makumi ya watu wameuawa katika mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Msemaji wa jeshi la Nigeria, Badare Akintoye amesema kuwa, mashambulizi mawili ya kigaidi yaliyofanywa na mawanawake wawili katika soko la mji wa Madagali kwenye jimbo la Adamawa yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 45 na kujeruhi wengine wengi. Akintoye ameongeza kuwa, kundi la Boko Haram ndilo lililopanga mashambulizi hayo.

Udhaifu wa jeshi la Nigeria na kushindwa kwake kukabiliana na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Boko Haram vinachangia sana katika mauaji ya maelfu ya raia wa nchi hiyo katika mashambulizi yanayoendelea kufanywa na magaidi hususan katika maeneo ya kaskazini yenye idadi kubwa ya Waislamu.

Image Caption

Siku chache zilizopita jumuiya mbalimbali likiwemo shirika la Amnesty International zilitangaza kuwa, wanawake na wasichana wa Nigeria waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram wanatumiwa katika mashambulizi ya kujilipua kwa mabomu. 

Ripoti ya Amnesty International imesisitiza katika ripoti yake kuwa, wanawake wengi wamekuwa wakimbizi kutokana na mapigano yanayoendelea katika maeneo hayo na wanalazimika kuuza miili yao kwa ajili ya kupata chakula.

Tags