Wanne wauawa katika mlipuko wa kigaidi Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i21289-wanne_wauawa_katika_mlipuko_wa_kigaidi_somalia
Mlipuko wa kigaidi uliotokea leo katika mji wa bandari wa Kismayo nchini Somalia umeuawa watu wanne.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 12, 2016 10:27 UTC
  • Wanne wauawa katika mlipuko wa kigaidi Somalia

Mlipuko wa kigaidi uliotokea leo katika mji wa bandari wa Kismayo nchini Somalia umeuawa watu wanne.

Polisi ya Somalia imetangaza leo kuwa, watu wasiopungua wanne wameaga dunia na wengine kumi kujeruhiwa katika mlipuko wa kigaidi uliotokea katika mji wa bandari wa Kismayo katika eneo la Upper Juba kusini mwa Somalia.  Abdalllah Farah, kamanda wa ngazi ya juu wa polisi ya Somalia ameongeza kuwa, watu wanne wanaoshukiwa kuhusika na mlipuko huo wa kigaidi wametambuliwa na kutiwa mbaroni. Kamanda Farah amesema tayari wameanzisha uchunguzi kuhusu washukiwa hao.

Mlipuko Kismayo Somalia, watu wanne wameuawa

Mlipuko mwingine wa bomu la kutegwa garini ulitokea jana Jumapili katika lango la kuingilia katika bandari ya Mogadishu mji mkuu wa Somalia na kuua watu 35 na kujeruhi wengine zaidi ya 50. Kundi la kigaidi la al Shabab lenye makao yake Somalia limetangaza kuhusika na mashambulizi yote mawili ya jana na leo.

Somalia inapambana na makundi ya wabeba silaha kwa muda wa miongo miwili sasa. Miaka mitano iliyopita kundi la wanamgambo wa al Shabab lilifukuzwa katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, hata hivyo kundi hilo lingali linaendeleza mashambulizi na hujuma zake dhidi ya wanajeshi wa serikali, wananchi wa kawaida na kuvilenga pia vikosi vya kigeni vya kudumisha amani nchini humo.