Magaidi watano waangamizwa kaskazini mwa Misri
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i26744-magaidi_watano_waangamizwa_kaskazini_mwa_misri
Magaidi wasiopungua watano wameuliwa na wanajeshi wa Misri katika eneo la Jabal al Hilal, kusini mwa mji wa al Arish, katika mkoa wa Sinai Kaskazini.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 23, 2017 03:11 UTC
  • Magaidi watano waangamizwa kaskazini mwa Misri

Magaidi wasiopungua watano wameuliwa na wanajeshi wa Misri katika eneo la Jabal al Hilal, kusini mwa mji wa al Arish, katika mkoa wa Sinai Kaskazini.

Televisheni ya Sky News imetangaza habari hiyo leo na kuongeza kuwa, jeshi la Misri limefanya mashambulizi katika maficho walipokuwa wamekusanyika magaidi ambapo wameripua pia ghala mbili za silaha za magaidi hao.

Polisi na wanajeshi wa Misri wamekuwa wakiendesha operesheni za pamoja za kupambana na makundi ya kigaidi tangu mwaka 2013 baada ya jeshi la nchi hiyo likiongozwa na Jenerali Abdul Fattah el Sisi, kufanya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Misri, Muhammad Morsi.

Wanajeshi wa Misri katika operesheni za kupambana na magaidi Sinai Kaskazini

 

Eneo la Sinai Kaskazini limekuwa likishuhudia mashambulizi ya mara kwa mara ya kundi la Ansar Baytul Muqaddas, tawi la genge la kigaidi la Daesh nchini Misri. Al Arish ndio makao makuu ya mkoa huo wa kaskazini mwa Misri.

Hadi hivi sasa kundi la Asnar Baytul Muqaddas limeshafanya makumi ya mashambulizi dhidi ya maeneo ya wanajeshi na raia wa kawaida wa Misri na kuua watu wengi sambamba na kuharibu miundombinu ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.